Search This Blog

Saturday, July 23, 2022

1

 Next Article WARAKA ULIOWAVUA VYEO ZITTO, DK KITILA NA MWIGAMBA HUU HAPA November 22, 2013, 10:17 am Zitto Kabwe. MKAKATI WA MABADILIKO 2013 UTANGULIZI: Taasisi tunayoizungumzia ilisajiliwa rasmi mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wakuu wa taasisi wapatao wawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Wa kwanza aliongoza kwa miaka mitano tangu wakati huo 1993 hadi 1998 na kumwachia aliyefuata ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzoni mwa 2004 na kumwachia aliyepo sasa. Huyu aliyepo aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwa tena mwaka 2009 kwa kipindi cha pili. Tunapenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wakuu wetu wote waliopita walizozifanya katika kuhakikisha taasisi yetu inakua kwa kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katika mazingira yaliyowakabili. Mwaka 1995 chini ya mkuu wa kwanza tulipata wawakilishi watatu kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi. Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa nyongeza mmoja na kufanya idadi kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya mkuu wa tatu ambaye ndiye aliyepo hivi sasa, tulipata wawakilishi watano na wa nyongeza sita jumla wakawa 11. 2010 chini ya mkuu huyu huyu wawakilishi wakaongezeka na kuwa 23 na wa nyongeza 25 na kufanya idadi kuwa 48 kabla ya kupata mwingine mwaka jana na kufanya sasa wawe 49. Dk. Kitila Mkumbo. Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwana taasisi. Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika mwongozo wetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika mwongozo bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu. Samson Mwigamba. Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Tunapenda kuainisha matatizo hayo kwa uchache kama ifuatavyo: Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa taasisi yetu. Ni dhahiri kwamba uongozi uliopo umeishiwa mbinu na kuakisi jambo la msingi sana ambalo waasisi wetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye mwongozo wetu. Kuchoka kwa uongozi wetu kunaonekana dhahiri katika mipango na mikakati ya taasisi ya miaka kadhaa. Mfano mwaka 2008 uongozi ulianzisha mkakati wa operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara). Huo ulifanyiwa kazi katika mikoa kadhaa na hatimaye ikafa kimya kimya. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwa yakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya zote. Kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na kwenda kwenye wilaya zote. Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba yalifanyika Mwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende. Kisha mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C). Hiyo ilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumla zilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa njia ya mikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye kufanya mafunzo kwa viongozi. Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na kisha ikaenda kufia Iringa. Mwaka huu viongozi wetu wamekuja na ugatuaji madaraka kutoka makao makuu ya taasisi na kupeleka madaraka kwenye kanda mbalimbali. Mkakati huu ulikufa kabla ya kuanza pale viongozi wakuu walipobadilisha maazimio ya kikao kikuu na kutekeleza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuleta suala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri maofisa na wakahakikisha wanaweka watu wao kwenye uongozi wa muda. Kitendo hiki kwa peke yake, cha kufeli kwa kila mkakati unaoletwa na viongozi wetu katika hatua za utekelezaji unaofanywa na wao wenyewe waleta mkakati, ni kiashiria tosha kwamba uongozi uliopo umechoka. Performance yetu kwenye chaguzi ndogo nayo ni ishara kwamba mabadiliko yanahitajika. Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8 za wawakilishi kwenye chombo kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na asilimia 25. Aidha baada ya mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za wawakilishi kwenye halmashauri. Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa4 2012, mwezi Septemba 2012 na mwezi Juni 2013. Kote performance yetu imekuwa poor kupindukia. Mfano mwezi wa Juni 2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi Septemba 2012 tulipata viti 7 kati ya 29 (24%). Ni dhahiri mabadiliko yanahitajika kwa kuwa wakuu waliopo wanatumia mbinu zile zile na kupata matokeo yale yale. Tunahitaji mbinu mpya. Kwa kifupi, ushindi ambao tumekuwa tukiupata katika chaguzi ndogo haulingani na ukubwa wa hamasa kwa taasisi yetu iliyopo mitaani. Hii ni kwa sababu tumekuwa tukitumia mbinu hizohizo katika kila chaguzi. Aidha, tu wepesi mno wa kuridhika na kujisifu kwa mafanikio madogo badala ya kukaa chini na kutafakari kwa kina mahala tunapojikwaa. Matumizi ya fedha za taasisi. Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable. Taarifa za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu tuliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama. Kwa kiasi kikubwa mkuu aliyepo anatengeneza mazingira yaleyale ya mwaka 2005 na 2010 ya kutaka chama kiwe hakina hela ili ikifika wakati wa uchaguzi kimpigie magoti. Kisha atatoa pesa bila kumbukumbu zozote na mara baada ya uchaguzi anapeleka lundo la deni na kudai alipwe hela aliyekikopesha chama wakati wa uchaguzi. Alifanya hivyo katika chaguzi za 2005 na 2010. Wakati wote wa kampeni za mwaka 2010, kwa mfano, taasisi yetu ilihangaika sana kwa kukosa hata hela ya kununua maji kwa wajumbe wa ngome. Lakini ajabu ni kwamba baada ya uchaguzi mkuu wa taasisi na baadhi wa wapambe wake walilete deni kubwa la takribani shililingi milioni mia tano akiadi kuwa walikikopesha chama. Taasisi imewalipa pesa zote hizi kwa muda mwaka mmoja. Sasa anatengeneza mazingira hayohayo kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama. Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama lile la kuanzisha kampuni la uwekezaji la taasisi yetu litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa hapa jirani juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote. Njia haramu za kubaki madarakani. Ili kuhakikisha wakuu wanabaki madarakani, wameanzisha vikundi vikundi ndani ya taasisi yetu. Siku hizi ni rahisi sana kuambiwa kwenye taasisi yetu eti huyu ni wa boss na huyu ni wa dogo. Na wale walio wa boss kwa kuwa boss ndo anashikilia raslimali za taasisi anatumia mfumo haramu kuwaneemesha watu wake kwa kutumia raslimali za taasisi na kuwakandamiza wote wanaoonekana wanapishana naye kimtazamo. Jambo hili limewaibua wachumia tumbo, wapenda madaraka, na vibaraka lukuki wanaokwenda kujipendekeza kwa wakuu wa taasisi kwa malengo ya kujinufaisha binafsi. Katika kufanya hivyo vibaraka hao wamekuwa wakiwaendea wakuu wa taasisi na kuwajaza maneno mabaya dhidi ya viongozi wenzao na kuzidi kuwafarakanisha viongozi wa juu. Kuna mchezo umeanzishwa na wakuu wa taasisi unaitwa ulinzi wa chama uliogawanyika katika makundi mawili yaani visible na invisible. Visible ni ule unaoonekana ambao uko chini ya kikosi chetu chekundu ambacho kinajulikana kwa kila mtu lakini invisible wanajulikana kwa mkuu wa taasisi na mtendaji mkuu peke yake. Wanafanya kazi kwa maelekezo ya wakubwa hao wawili na hawajulikani kwa viongozi wengine wa juu. Ni hawa hawa ambao wanatumika vibaya pale wanapoleta taarifa za kiintelijensia ambazo zinawahusisha viongozi wasiopendwa na wakuu na usaliti dhidi ya taasisi. Hakuna kamati maalum inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka. Ni katika mfumo huu wa kipuuzi mida eight amekuwa akitumika vibaya kwa kumshambulia mtendaji mkuu msaidizi hadharani kwa kutumia mitandao ya kijamii na wakuu wanafurahia na kumlipa pesa. Udhaifu wa utendaji wa mtendaji mkuu. Mtendaji mkuu ni dhaifu mno na ni mara nyingi sana tumeshuhudia mkuu wa taasisi akifanya mambo ya kiutendaji kinyume na utaratibu kama vile yeye mwenyewe kuja kwenye kamati ya makatibu na wakurugenzi na kupangua mipango yao na ku-inject ya kwake na mtendaji mkuu kuadopt tu kana kwamba yeye hawezi kupanga mambo ya kiutendaji, hata tunapokuwa kwenye operesheni maalum tumeshuhudia mkuu wa taasisi ndo akipanga watendaji, posho zao na hata kusimamia matumizi ya pesa na shughuli mbalimbali za kiutendaji. Udhaifu wa mtendaji mkuu ni udhaifu wa mkuu wa taasisi kwa kuwa amemteua yeye mara mbili tena mara ya pili alileta jina moja mbele ya Baraza la juu kuonyesha kwamba aliridhika na utendaji wake kiasi cha kutotaka kumpambanisha na mwingine. Lakini baada ya kumpendekeza mara ya pili ndipo tumeshuhudia yeye kuingilia kati mara nyingi sana mambo ya kiutendaji kana kwamba anamfichia aibu mtendaji wake. Swali kwa nini alimteua tena? Jibu lake litakuwa rahisi tu kwamba ni kwa sababu mtendaji huyu ni passivekwa kila takwa la mkuu wake. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi. Taasisi yetu inayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya kamati ya makatibu na wakurugenzi. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu, wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, vifaa vya kueneza taasisi, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa mtendaji mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yote yanafanywa na wakuu hasa hasa mkuu wa taasisi bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Bila aibu, mkuu wa taasisi ndio amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambaye haihojiwi popote. Huu ni mfano wa wazi wa mgongano wa kimaslahi jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi mkubwa wa taasisi kama yetu inayojitambulisha katika kupinga vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa maadili ya uongozi kwa ujumla. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya kueneza taasisi. Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu. Mifumo ya uteuzi wa maofisa wa makao makuu ya taasisi imevurugwa na siku hizi wakuu wa taasisi hasa mtendaji mkuu anateua na kutimua ofisa anavyotaka na mara nyingi bila hata kamati ya makatibu na wakurugenzi kujua. Mambo haya yanafanyika mbele ya macho na masikio ya mkuu wa taasisi jambo ambalo linazidi kuthibitisha kwamba mkuu na mtendaji mkuu wanajuana na wanafanya kwa kulindana. NANI TUMUUNGE MKONO KUCHUKUA NAFASI YA MKUU: Baada ya utangulizi huo unaoonyesha kinagaubaga kwamba tunahitaji mabadiliko, hatua iliyofuata ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta mabadiliko tunayohitaji. Ni vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye tungemuunga mkono lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko tunayetaka kumtoa. Awe ana qualities za kiuongozi na zaidi sana awe na uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko. Tukileta mtu asiyefahamika sana kwenye mifumo ya taasisi yetu hata kama angekuwa mzuri kiasi gani hatachagulika na mkuu aliyeko atarudi kwa urahisi na kuendelea kuididimiza taasisi. Katika kuchunguza ndani ya taasisi tuliridhika kwamba mtendaji mkuu msaidizi ana sifa zote tulizozitaja hapo juu ingawa kila mwanadamu ana udhaifu wake. Ni dhahiri pia kwamba udhaifu wa mtendaji mkuu msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu aliyepo. Kwa ujumla mtendaji mkuu: Ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi ya taasisi kuliko maslahi binafsi. Ameonyesha kwa vitendo kwamba hana maslahi binafsi kwa kuwa tumeshuhudia akifanya kazi nyingi za taasisi bila kudai malipo kwa njia ya posho ama vinginevyo. Anaheshimika na viongozi wa ndani na nje ya taasisi jambo ambalo ni la muhimu sana kwa ustawi wa taasisi na kwa yeye kuwa mkuu wa taasisi tunatarajia wakubwa wengi sana kutoka nje ya taasisi yetu kuiamini na hata kujiunga nasi katika kuhakikisha tunafanikisha lengo la taasisi. Ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimichezo, nk jambo ambalo ni muhimu sana kwa kuwa ni hatari kuwa na kiongozi asiye na ujuzi wa kutosha kwenye masuala kama hayo. Ndani ya taasisi anakubalika kwa makundi yote ya vijana, wazee na akina mama. Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara. Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo. Uelewa wake wa mambo ya kiuchumi ni muhimu sana kwa taasisi kwa sasa. Tunahitaji kuja na vyanzo vipya vya mapato ikiwa tunahitaji kufanikiwa. Mkuu aliyepo si kwamba ameishiwa bali hana mbinu za maana za kuiimarisha taasisi kimapato kwa ajili ya malengo yake ya mbele. Exposure kubwa na kukubalika katika siasa za kimataifa. Tunahitaji kiongozi ambaye anazifahamu siasa za kimataifa na anayeweza kuungwa mkono na viongozi wengi wa kimataifa. Ni hatari kutegemea utaweza kufanikisha malengo kama ya taasisi yetu bila mpango kabambe wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa. Mpaka hivi sasa hakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na jumuia ya kimataifa. Kiongozi wetu mkuu wa sasa yupo ‘too local’ na hana mawasiliano yeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na kimataifa. Ndio maana mkuu huyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa hawaonekani katika matukio makubwa ya kimataifa. Hata katika kutoa maoni katika mambo makubwa ya kitaifa na kimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa kifupi kwa sababu ya aina ya viongozi tulio nao, nafasi ya taasisi yetu katika nyanja za kimataifa haipo! Aina na staili ya uongozi wa sasa wa taasisi yetu ni kina kwamba nchi hii haipo hadi taasisi yetu itakapochukua dola. Yaani tunafanya mambo kama kwamba tutaanza upya kabisa tukichukua dola. Ni kwa sababu tumegombana na kila mtu katika utawala wan chi, vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba tutavihitaji vyombo hivi kabla na baada ya kuingia madarakani na ni ndoto kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwa kugombana na kila mtu. Ni kwa sababu ya mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetu wa sasa hawaonekani kabisa katika shughuli za kitaifa kama vile sherehe za uhuru wan chi, n.k. Uwezo wa kuwaunganisha wasomi wa kada mbalimbali, wafanyabiashara wakubwa, watumishi wa umma na sekta binafsi, nk katika kupata muunganiko wa mawazo na kutoka na sera murua zinazogusa kila sekta. Hili la kuwashirikisha litaenda sambamba na kutoa elimu kwa wote waelewe na watuunge mkono. Tunasema hivi kwa kuwa watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi,nk na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo. Kubwa zaidi ni kwamba alishaiangalia taasisi yetu na kuona mambo yanayohitaji mabadiliko na kujiangalia yeye na kuridhika kwamba ataweza kuleta mabadiliko tunayoyahitaji na ndipo mwaka 2009 aliamua kujitosa kuutafuta ukuu wa taasisi yetu kabla ya kuombwa kumwachia aliyepo. SWOT ANALYSIS: Kwa kutumia uchambuzi huu hapa chini wa uimara, udhaifu, fursa na vitisho ama vikwazo dhidi ya mtu tunayempendekeza, utaweza kutuonyesha kama tunayempendekeza ataweza kushinda vita iliyo mbele yetu. Kama SWOT inavyotaka, tutaangalia sifa njema alizonazo tunayemtaka ambao ndio uimara wake, tutaangalia pia udhaifu wake, tutaangalia fursa alizonazo na mwisho tutazingatia vitisho ama vikwazo vilivyopo. Ni muhimu tukaeleza kwamba katika SWOT analysis tunajikita kwa mambo yanayohusika moja kwa moja na uwezekano wa tunayemtaka, kuchaguliwa. Kwa hiyo kwa mfano utakuta kwamba katika sehemu hii hatutazungumzia sifa njema alizonazo tunayemtaka kama kiongozi lakini sifa hizo zikawa hazina ushawishi wa kuwafanya wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua. Uimara wa tunayemtaka: Ingawa si mmoja wa waasisi wa taasisi yetu, lakini ni mwana taasisi mkongwe akiwa amejiunga na taasisi yetu miaka miwili tu tangu ianzishwe na mwaka mmoja tangu isajiliwe rasmi na serikali. Zaidi ya kuwa mwanataasisi mkongwe, hajawahi kujiunga na taasisi nyingine hapo kabla. Alijiunga na taasisi hii kabla hata haijajulikana kwa watu na alibaki kuwa mwana taasisi mwaminifu hata pale taasisi zingine zilipoonekana kuwa imara na maarufu zaidi ya hii. Kutokana na vipengele ‘a’ na ‘b’ hapo juu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kusema mtu huyu alikuja kwenye taasisi yetu kwa ajili ya kutafuta maslahi kama vile uwakilishi kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi hapa nchini. Ni mvumilivu sana. Katika jitahada za wakuu waliopo kuhakikisha wanaendelea kukalia viti vyao, wamejitahidi sana kumpaka matope lakini amevumilia. Mahali ambapo wengine wangeshakata tamaa na kuhama taasisi, yeye alibaki kuvumilia mpaka imefikia wana taasisi wa ngazi za chini waliokuwa wanadanganywa kwamba mtu huyu ni msaliti, wameanza sasa kushtuka. Ana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi. Ana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Uwezo wake unachagizwa si tu na elimu yake ya darasani bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa. Ni mzalendo wa hali ya juu anayeipenda nchi yake kwa moyo wa dhati. Amethibitisha hilo kwa namna anavyolitetea taifa letu katika medani za kimataifa na jinsi anavyolipigania ndani dhidi ya mafisadi na wasiolitakia mema taifa letu. Ni mwakilishi pekee aliyekuwa tayari kukosa mishahara ya miezi kadhaa kwa kuamua kusimamia ukweli kwamba kuna ufisadi ulifanyika mpaka akasimamishwa uwakilishi wake kwa mikutano kadhaa ya chombo chetu cha uwakilishi. Katika kuzidi kuonyesha alivyo mzalendo tunaweza kusema hapa kwamba ni kiongozi pekee kutoka upande huu ambaye ameonekana sana kwenye mambo ya kitaifa kwa mfano kulipigania taifa letu katika mambo ya kimchezo, kutumia gharama zake kwenda nje ya nchi na kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kulisaidia taifa katika sekta nyeti kama mafuta, gesi na madini, nk bila kusahau kwamba amekuwa ndiye mwakilishi pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za ubadhirifu ndani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi. Mambo hayo tuliyoyataja kwenye vipengele ‘e’, ‘f’, ‘g’ na ‘h’ yamemfanya kuwa kiongozi wa kwanza kuwa maarufu sana katika taasisi yetu aliyewapiku hata viongozi wa serikali kwa umaarufu. Hii ya umaarufu ni sifa muhimu sana linapokuja suala la uchaguzi. Uwezo wake wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi. Hata pale anapokuwa amepakwa sana matope na wenzake, anapopewa nafasi ya kujieleza huweza kuwashawishi watu wengi wanaomsikiliza. Hii itamsaidia sana siku ya kujieleza mbele ya kikao cha uchaguzi ambapo ataweza kupangua hoja zote dhaifu za kumpaka matope. Ana uwezo wa kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama mwenzao, wanawake humwona kama mtetezi wao wakati wazee humwona kama kijana mwenye busara anayeweza kuelekeza kama kiongozi. Ana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na ziara nyingi alizozifanya na kukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Mahusiano haya mazuri yanachagizwa na jinsi anavyotumia muda wa kuongea na viongozi wa ngazi za chini kuzungumza kwa lugha ya upole na kuelekeza viongozi wenzake bila kuwaonyesha dharau. Si mtu wa kujipenda nafsi na katika kupambana umaskini wa watu badala ya umaskini wake, alifikia kuzikataa posho wanazolipwa wawakilishi wakati wakitekeleza majukumu ambayo kwayo wanalipwa na kuiomba ofisi ya chombo hicho kuzipeleka posho hizo kwa watu maskini. Ana limu nzuri sana aliyoipata katika vyuo vinavyoeleweka kitaifa na kimataifa Ni kijana na hii ni taswira njema kwa sababu taasisi yetu inaungwa mkono sana na vijana Udhaifu wa tunayemtaka: Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu. Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake. Hali ya ndoa ya tunayemtaka kutoeleweka msimamo wake Kuna wakati tunayemtaka hu-respondkwa taharuki kubwa dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka huonekana kufanya maamuzi kwaemotion zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kurespond. Jambo lililoelezwa katika ‘d’ hapo juu humfanya tunayemtaka wakati mwingine kuonekana ana jazba sana kwa sababu akishataharuki na kuchukua maamuzi akingali kwenye taharuki huwa ni rahisi sana kuonekana anajibu mapigo kwa jazba sana. Ustahimilivu: yaliyotajwa katika ‘d’ na ‘e’ hapo juu yanaashiria tunayemtaka si mstahimilivu sana sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi. Uwazi: Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza. Fursa alizonazo tunayemtaka: Utamaduni wa taasisi yetu wa kubadilisha wakuu wa taasisi kila baada ya vipindi vifupi ili kuleta maono mapya kwenye taasisi unampendelea tunayemtaka. Udhaifu ulioonyeshwa na uongozi uliopo chini ya mpinzani wetu katika kutekeleza program mbalimbali za taasisi nyingi zikiwa zimebuniwa na wao wenyewe, pia ni fursa kwa tunayemtaka. Udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na uongozi uliopo kwenye ugawanyaji wa raslimali za taasisi kama vile fedha za ruzuku, michango mbalimbali ya wahisani na hata vifaa vya uenezi. Kujitokeza kwa tunayemtaka kutaonekana kama fursa kwa wanataasisi kufanya mabadiliko makubwa na kuua kabisa ile propaganda ya kwamba taasisi yetu ni ya kabila fulani ama eneo fulani kwa kufanya reference kwa uongozi wa taasisi. Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka. Imani ambayo wana taasisi wengi wanayo kwake. Utafiti mdogo unaonyesha kwamba bado jina la tunayemtaka linatamkika sana midomoni mwa wanataasisi pale wanapotajwa viongozi wa juu wa taasisi yetu. Hii inaonyesha bado wana taasisi wanayo imani kubwa kwake na kwa hiyo atakapopata fursa ya kupangua matope aliyopakwa atakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa. Mpinzani wetu hana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi. Hakuonyesha utendaji wowote wa pekee alipokuwepo kwenye chombo mwaka 2000 -2005 na hata alipopewa uongozi wa upande wetu ndani ya chombo tokea 2010 hadi leo 2013 hajafanya lolote la kutukuka ndani ya chombo hicho. Mpinzani wetu hana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake. Uzalendowampinzani wetu unatia shaka akiwa hajaonyesha lolote la maana katika kulitetea taifa letu kimataifa. Ingawa ameshapata nafasi lukuki ya kwenda nje ya nchi lakini mara zote akifika huko ni kuiponda tu nchi yake. Ingawa anayo majukwaa ya kufanya hivyo akiwa ameshakuwa mwakilishi mara mbili kwenye chombo chetu lakini hatujawahi kumsikia akiibua kashfa mahsusi ya ufisadi na kuisimamia zaidi ya yeye mwenyewe wakati fulani fulani kutuhumiwa kwa ufisadi mfano pale alipokopa kwenye shirika la umma na kugoma kulipa mkopo. Katika kuzidi kuonyesha uzalendo hafifu wa mpinzani wetu tunaweza kuangalia jinsi ambavyo mpinzani haonekani kwenye mambo ya kitaifa. Hii ni fursa kwa tunayemtaka. Mpinzani wetu si maarufu akilinganishwa na tunayemtaka na hivyo kumpa fursa zaidi tunayemtaka kumshindani mpinzani wetu kwenye uchaguzi. Uwezo wa mpinzani wetu wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi ni mdogo sana. Mpinzani wetu hajazoea ushindani na changamoto. Ni mtu aliyezaliwa kwenye utajiri na anadhani pesa ni kila kitu. Ukimnyang’anya pesa ukamwambia ashindane kwa hoja hawezi na ndo maana anajaribu sana kuhakikisha anaingia mwenyewe ulingoni bila kupingwa. Kutokana na tuliyoyasema hapo juu kwenye ‘m’ ni dhahiri kwambapale mpinzani wetu anaporushiwa kombora la kashfa anakuwa mzito kujieleza hata kama anapewa nafasi ya kufanya hivyo na hii ni fursa muhimu kwa tunayemtaka. Mpinzani wetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwake tu bali hata za watu wengine. Mpinzani wetu hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Hutumia muda mwingi kuwaponda viongozi wenzake hata kufikia kutamka mara nyingi kwamba kama kiongozi hawezi kujigharamia nauli na malazi ya kutoka mahali fulani kwenda mahali fulani kwa siku kadhaa hafai kuwa kiongozi bila kujali kwamba kuna viongozi wetu wana moyo na taasisi hii na ndo wameifikisha hapa ilipo lakini hawana uwezo wa kifedha na hivyo kauli kama hizo za mkuu huyu huona kama anawadharau kwa kuwa yeye ni tajiri. Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi ya chini hivi sasa na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka. Mkuu aliyepo amekuwa na mkakati unaoitwa kuondoa watu wa zamani. Jambo hili linawaudhi sana viongozi wa ngazi za chini ambao wanaona kama baada ya kuifikisha taasisi mahali ilipo kwa sasa wanaonekana hawana maana tena. Wengi wamefikia kuapa kwamba kama mwendo ni wa kuwaondoa watu wa zamani basi na yeye ni wa zamani lazima aondoke. Mpinzani wetu amejionyesha dhahiri kujipenda na kujijali nafsi bila kujali watu wa hali ya chini. Matukio mawili yanamwacha uchi katika hili pale alipolitangazia taifa kwamba wawakilishi wetu wote hawatachukua posho za vikao halafu yeye na wengine wote wanazichukua hadi leo na kumwacha mtendaji msaidizi peke yake. Na la pili linalofanana na hilo ni pale alipotangaza kutotumia gari la serikali ambalo ni la kifahari kisha akalirudia kimya kimya. Kuwepo muhtasari wa kikao cha wazee ambacho mwaka 2009 kilimshauri tunayemtaka ajitoe na kumwachia mkuu aliyepo na kumtaka mkuu aliyepo kumwachia tunayemtaka katika uchaguzi ujao na wote wakasaini makubaliano hayo, nayo ni fursa muhimu sana kwa tunayemtaka. Mkuu aliyepo anaamini kwamba ameshamsambaratisha tunayemtaka na hivyo kwa sasa amebweteka na hiyo inatupatia sisi fursa kuendelea kuimarisha mtandao wetu. Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu. Elimu ndogo na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu kwa sasa. Kwa sasa ni kiongozi pekee katika nchi yetu anayeongoza taasisi kubwa asiye na elimu ya shahada huku taasisi yetu ikiwa inaongoza kwa kuwa na wasomi waliobobea katika kila nyanja. Hii ni kejeli hasa kwetu sisi ambao tumekuwa tukiwasema wenzetu kwamba ‘akili ndogo’ inaongoza akili kubwa. Kimsingi tumekuwa tukijisema kwa kukubali kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo. Mkuu wa sasa kutokuwa na msimamo thabiti katika mambo ya msingi. Rejea swala la maandamano ya kumshinikiza Kawambwa ajiuzulu na kujitoa katika mchakato wa katiba. Vikwazo dhidi ya tunayemtaka: Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious. Utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote Kitendo cha mkuu aliyepo kung’ang’ania kuendelea nayo ni kikwazo kwa kuwa baada ya kuwa madarakani kwa miaka yote hiyo lazima amejipatia watu wanaomhusudu ama kumpenda ama kumkubali na kuwepo wengine wanaoogopa tu kwamba mkuu aliyepo akitoka taasisi itakufa hata kama hawana sababu yoyote. Tunatazamia mkuu aliyepo atafanya vitendo vingi zaidi vya haramu katika kumdhibiti tunayemtaka pale tunapoelekea kwenye uchaguzi wenyewe. Raslimali za taasisi kutumiwa na viongozi waliopo katika kumsaidia mkuu aliyepo wakati wa kwetu anatumia raslimali zake za mfukoni. Propaganda chafu zilizokwishapigwa dhidi ya tunayemtaka zimepunguza imani ya wanataasisi kwa tunayemtaka kwa kiasi fulani Baadhi ya mambo ambayo amekwishayasema ama kuyatenda nayo yameshawapunguzia imani kiasi fulani wanataasisi mbalimbali. Kutoonekana sana kwenye operations za taasisi yetu pia kumewapa wasiwasi baadhi ya wanataasisi. Muhtasari wa SWOT analysis unaonyesha kwamba strength na opportunities za tunayemtaka ni nyingi sana zikilinganishwa na weaknesses zake na threats dhidi yake. Aidha ukichambua zaidi utaona kwamba weaknesses za tunayemtaka nirepairable na vikwazo dhidi yake pia ni rahisi kuvikabili na kuvisambaratisha. Tukishamaliza maandalizi ya mkakati huu tukaonana na mhusika mkuu na kumpa ushauri akatulia na kufanya kazi, mkuu aliyepo hatafua dafu. Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndiyo maana hata lugha iliyotumika ni ndani hapa ni ya pekee. Tunahitaji tunayemtaka asionekane kama kuna kitu anafanya na tunafurahi kwamba kuna wakati alitangaza kwamba hana nia ya kugombea tena waliopo wanatosha. Ikitokea vyombo vya habari vikamuuliza tena hiyo ndiyo iwe kauli yake ili kuendelea kumfanya mkuu aliyepo asihangaike na hivyo kuja kummaliza kirahisi. Aidha katika utekelezaji wa mkakati kama tutakavyoeleza hapo baadaye, tunayemtaka atajitenga mbali asionekane hata kuwa karibu na sisi. Vikao vyetu na yeye vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani. Mkakati huu hautatakiwa kupatikana kwenye komputa zaidi ya tatu yaani ya mchapaji ambaye ni M3, ya M3 na ya MK mwenyewe. Hata hivyo email zitakazotumika kusafirisha mkakati huu kutoka kwa M3 kwenda kwa M1 hadi kwa MK hazitakuwa zile za kawaida za hao watu bali mpya kabisa zilizofunguliwa kwa makusudi haya tu na kwa majina fictitious. Aidha kila atakayekuwa na mkakati huu kwenye computer yake anatakiwa kuliwekea file hilo password ili hata mtu wa karibu naye anayeweza kufungua computer yake asiweze kulifungua file hilo. Pia email address hazitatolewa kwa sms bali kwa kupiga na kuambiana spelling za address. MTANDAO WA USHINDI: Mtandao wa ushindi utakuwa kama ifuatavyo. Kwenye ngazi ya kitaifa tutakuwa na kamati yenye members watatu tu. M1 ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa. M2 ni mtu ambaye yuko kwenye ofisi kuu za taasisi yetu wakati M3 ndiye mchapaji wa mkakati huu. Kamati hii imefanywa kuwa na members wachache sana wenye uelewa mpana wa mambo na wenye elimu nzuri ili kuhakikisha kazi inafanyika kitaalam na kwa uhakika sana. Kamati ya kitaifa itapeleka mapendekezo yake kwaMM na yeye pia ataleta ushauri wake kwa kamati kama mishale inavyoonyesha. Chini ya kamati ya kitaifa kutakuwepo waratibu wa kanda zote kumi watakaojulikana kama MK1 – MK10. Hawa watatafutwa na kusimikwa na kamati ya kitaifa kwa kushauriana na MM kwa utaratibu utakaokubalika na pande zote yaani MM na kamati ya kitaifa. Chini ya waratibu wa kanda kutakuwapo waratibu wa mikoa yote 30 (MMK1 – MMK30) ambao watapatikana kwa utaratibu ule ule wa kuwapata waratibu wa kanda. Isipokuwa pale ambapo inakuwa ngumu, itabidi kamati ya taifa isaidiane na waratibu wa kanda kuwapata waratibu wa mikoa lakini kamati itashauriana na MM kabla ya kuwasimika rasmi hao waratibu wa mikoa.Mtandao utakuwa kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro ufuatao: NAMNA YA KUFANIKISHA MKAKATI: Kazi itagawanywa katika awamu tatu: Awamu ya kwanza ni kuanzia sasa mpaka uchaguzi wa ngazi ya matawi utakapoanza. Katika awamu hii kazi ni kuhakikisha kwamba mtandao mzima umekamilika mpaka kwenye ngazi ya mkoa. Kazi nyingine itakayofanyika ni kwa waratibu wa mikoa kuendelea kuspot makada kwenye wilaya na mikoa ambao tayari wana mtazamo tulio nao ama ambao wanaweza kuingiziwa kirahisi mbegu hii ya mabadiliko na wakawa tayari na wana uwezo na sifa za kushinda uongozi kwenye wilaya na mikoa yao bila kusahau sifa ya kuwa waaminifu wenye uwezo wa kutunza siri. Kulingana na muda hii ni kazi inayotakiwa kufanyika sasa lakini kwa uangalifu mkubwa. Ni muhimu kukumbushana hapa kwamba katika awamu hii hakuna anayetakiwa kujua mpango mzima zaidi ya kamati ya kitaifa na MMili kuhakikisha uwezekano wa mkakati wetu mapema kwa wapinzani wetu unakuwa minimized to almost zero. Awamu ya pili ni kipindi kuanzia uchaguzi wa matawi mpaka uchaguzi wa mikoa unapokamilika. Katika awamu hii tutasaidiana na waratibu wa kanda na mikoa kuhakikisha makada tuliowaspot kwenye wilaya wanapanga safu zao kwenye kata ili kuhakikisha watakaochaguliwa kwenye kata ni watu wao ili waje wawachague kwenye wilaya.Vivyo hivyo kwa makada tuliowaspot kwenye mikoa wahakikishe wanaochaguliwa kwenye wilaya ni wale makada wetu ili nao waje wawachague kwenye mikoa yao. Hapa ndipo kwenye kazi kubwa ya mkakati wetu na hapa ndipo tutakapohitaji kuingia gharama zaidi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia angalau 80. Awamu ya tatu ni kuanzia baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mikoa hadi uchaguzi wa kitaifa utakapoitishwa. Katika kipindi hiki kwa ustadi mkubwa tutakuwa tukiwaandaa makada wetu waliochaguliwa tayari kuja kufanya mabadiliko makubwa kitaifa. Ni wakati huu ambapo tutawaingizia mkakati taratibu lakini kwa ustadi mkubwa tukijikita hasa kwenye kuonyesha kwa nini tunahitaji mabadiliko. Ni katika kipindi hiki ambapo kwa ustadi mkubwa tunaweza kuwaspot wale waliochaguliwa ambao hatukuwaandaa na kuwaingizia pia mbegu ya mabadiliko ili kuwawin na kuwarecruit kwenye mkakati. Aidha katika awamu zote tatu kazi ya kuianalyze ofisi kuu itakuwa non stop kwa kuzingatia kwamba mabadiliko ya wakurugenzi na maofisa yatakuwa yanatokea na watu nao watakuwa wanabadilika kimtazamo. Analysis ya ofisi kuu ni kuhakikisha tunajua nani na nani wako na sisi na nani na nani wako against na pia nani na nani wanaweza kupandikiziwa mbegu kwa ustadi na wakaungana nasi. MAHITAJI YA KUFANIKISHA MKAKATI: Raslimali watu. Tunahitaji watu waaminifu watatu kwenye ngazi ya kitaifa ambao tayari wapo. Tunahitaji watu waaminifu kumi kwenye kanda ambao tutawatafuta na pia waaminifu wengine 30 kwenye mikoa yote thelathini. Fedha. Tunahitaji fedha kwa ajili ya mawasiliano kati ya wanakamati na wale wa ngazi ya chini. Aidha tunahitaji fedha kwa ajili ya gharama za usafiri pale tutakapohitaji kwenda kwenye kanda na mikoa husika kwa ajili ya kusimika watu hao tunaowahitaji. MAPENDEKEZO MAHSUSI NA HITIMISHO: Katika kuhitimisha tunapendekeza mambo mahsusi yafuatayo: Kuhusu Bajeti: Tunapendekeza kwamba bajeti ya mkakati huu isipangwe hivi sasa. Ni muhimu tu sote kuelewa kwamba wakati wenzetu wanatumia raslimali za taasisi kujijenga na kutekeleza mkakati wao wa ushindi, sisi tunapaswa kuingia mifukoni. Kwa kila kila mmoja wetu atakuwa budget conscious ili kuepuka matumizi makubwa ya pesa. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba lazima pesa inahitajika ni muhimu M1 na MM kujaribu kuangalia namna ya kuraise pesa na kushauri. Otherwise, tutakapokuwa tunahitaji kufanya hatua yoyote ama jambo lolote tutakuwa ndo tunapiga hesabu za funds tunazohitaji kwa jambo husika na kuingia katika utekelezaji. Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa: Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa: Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge. Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk. Aendelee kushusha ‘nondo’ ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa. Ajitahidi kudhibiti jazba hata pale anapokuwa amebambikiziwa tuhuma nzito namna gani. Atulie, ashauriane na wazee ili kuona namna nzuri ya kujibu tuhuma zinazomkera. Tukumbuke kwamba wakati mwingine kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kuliko hoja nzito. Sambamba na ‘iv’ hapo juu, adhibiti sana emotion ili kuhakikisha kila kitu kinachofanywa ama kuzungumzwa kinachomgusa asikimbilie kuongea na vyombo vya habari ama kwenye mitandao ya kijamii bali afuate kile tulichokizungumza kwenye kipengele cha ‘iv’ hapo juu. Kuhusu mapambano ya kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii: Katika hili sisi hatukuona haja ya kufanya hivyo kwa sababu mbili: Imani yetu kwamba taasisi yetu ni kubwa kuliko watu kwa hiyo ni muhimu kuzingatia kwamba hatuiui taasisi katika mapambano haya. Tukiendekeza mashambulizi kwa njia ya mitandao ya kijamii hatutakuwa na ngao ya kuwakinga watu wa kawaida (wanataasisi na wasio wanataasisi) dhidi ya kujikuta wakiamini kwamba taasisi hii nayo haina jipya ni sawa tu na ile tunayotaka kuitoa. Tutakuwa tumeiua taasisi na mkakati huu hautakuwa na maana sana kama lengo ni kufanya mabadiliko ya uongozi wa taasisi tu lakini malengo ya taasisi ya mwaka 2015 yasitimie! Kujikita kwenye mashambulizi kupitia mitandao ni kuzidi kuwashtua wakuu waliopo kwamba bado tuko serious na mkakati wa kuwatoa na kuwafanya wafanye kazi zaidi huku wakiendelea kumpaka matope MM kwamba ndiye anayerusha makombora hayo kwenye mitandao kwa kusudi la kuhujumu taasisi maana hiyo ndo lugha yao. Hatukatai kwamba wakuu wanajua kabisa kwamba bado MM ana nia ya kumvaa mkuu aliyepo lakini tunajua kwamba kwa sasa wanaamini wamemdhoofisha na hana madhara tena. Ndiyo maana tunataka kutekeleza mkakati wetu kwa siri sana ili wafikiri MM amekata tamaa kumbe ndo anakuja na mkakati mzito zaidi. Hata hivyo, ni muhimu kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea! Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ‘ars’ na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi. Atakayefanya kazi hiyo ni sisi wengine wala si yeye! Pia tutahakikisha kila post ya kumchafua inapatiwa majibu bila kutumia ID yake inayojulikana. Ni vema aidha akatupatia majibu na sisi kuyapost ama afungue ID mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo kwenye mitandao halafu ndo awe anazitumia kujibu lakini kwa kuzingatia tuliyokwishayazungumza hapo juu yaani kutofanya kwa emotion na kuepuka jazba lakini pia kushauriana na watu wa karibu kabla ya kutoa majibu kwa jambo lolote linalomhusu. Kuhusu kamati ya kitaifa (hususan M2 & M3): Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo. Ni katika mwendelezo huo huo tunamwona M2 naye akiwa ukingoni kupigwa nje na kuachwa mtupu na wakuu waliopo katika kile wanachokiita wao reshuffle ya ofisi kuu. Kwa sababu hiyo tukapendekeza kwamba MM kwa kushirikiana na M1 kwa hatua ya kwanza wanaweza kutafuta kiasi cha sh. 2m kila mmoja tukijua kwamba kama members hawa wawili wakisaidiwa milioni mbili mbili wanaweza kuanzisha projects ambazo zitawasustain hata kama hawana ajira. Kwa hatua ya baadaye tutasaidiana kuona kama hawa members wanaweza kusecure good employments mahali, provided hazitawazuia kufanya siasa. Previous Article Next Article MWIGULU NCHEMBA:KUVULIWA VYEO ZITTO KABWE"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATWALA AKILI KUBWA" November 22, 2013, 10:19 am Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa, 1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu, 2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja, 3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake 4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu. Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa. Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list. I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi CHANZO NI BLOG YA MWIGULU NCHEMBA Previous Article Next Article BABU SEYA:ALIA DUNIA HAINA HURUMA, KUFIA JELA! November 22, 2013, 6:48 pm Hukumu iliyokaziwa na Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam, juzi (Alhamisi), ikipigilia msumari adhabu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya mwanamuzi mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesababisha maumivu makali kwa wahusika. Mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha'. Uthibitisho wa hilo unatokana na kauli ya Babu Seya, aliyoitamka mahakamani akimnong’oneza Papii Kocha, akisema: “Kweli hii dunia haina huruma, hukumu hii imeniuma sana kuliko zote ambazo zimetangulia.” Akizungumza kwa upole kwa sauti ya majonzi, huku sura yake ikionesha dhahiri kutokuwa  na furaha, Babu Seya aliendelea: “Kinachoniuma zaidi ni wewe, nakusikitikia sana, wewe ni kijana mdogo ambaye ulipaswa kuwepo uraiani ukitimiza ndoto zako na ukiisadia nchi yako. ...Akiwa katika huzuni na majonzi makubwa. “Ndoto zako zimeishia hapa. Tumejitahidi sana kukwepa hiki kifungo lakini imeshindikana, wewe unajua.” Hata hivyo, wakati akitoka nje ya ukumbi wa mahakama, Babu Seya alimweleza mwandishi wetu: “Hili jambo sijalifanya, nitaendelea kupambana mpaka mwisho.” NI HUKUMU YA MWISHO Msajili Mwandamizi wa Mahakama, Zahra Mruma, akisoma hukumu  hiyo alisema: “Ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao ni Jamhuri, umeendelea kuwa na nguvu, kwa hiyo vipengele vya utetezi vilivyowasilishwa na mawakili wa utetezi vimekosa nguvu ya kutengua hukumu ya awali.” ...Ndugu na jamaa wakiangua kilio baada ya hukumu. Zahra, alisoma hukumu hiyo kwa niaba ya jopo la majaji watatu ambao waliipitia upya hukumu hiyo, baada ya mawakili wa utetezi, Mabere Marando na Gabriel Mjele, kuomba Mahakama ya Rufaa ifanye mapitio ya mwisho, baada ya kutokuzikubali zote zilizotangulia. Mawakili wa upande wa utetezi, walitaka mapitio hayo yafanyike kwa hoja kwamba haiingii akilini kwa Babu Seya na mwanaye kushiriki tendo la mapenzi kwa pamoja, tena kwenye nyumba wanayoishi. Hoja hiyo ilishibishwa na maelezo kuwa Babu Seya na Papii ni Waafrika, kwa hiyo kitamaduni haiwezekani kushiriki mapenzi kwa pamoja. Utetezi mwingine ni kuwa nyumba ya tukio ni ya kifamilia, kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa tendo husika kutendeka, maana wengi wangekuwa wanashuhudia. KESI YA MSINGI Babu Seya na Papii, walishtakiwa na baadaye kukutwa na hatia ya kuwabaka, kuwalawiti na kuwaambukiza Virusi Vya Ukimwi, watoto nane, wenye umri wa kati ya miaka saba na sita. Mahakama ilielezwa kuwa Babu Seya alikuwa akiwaita watoto hao na kuwanunulia pipi kisha kuwaingiza ndani ambako waliwaingilia kwa zamu na baada ya kitendo, waliwapa mgao wa kati ya shilingi 100 na 150. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na mwaka 2004, hukumu ilitolewa, ikiwatia hatiani Babu Seya na wanaye watatu na kuwahukumu kwenda jela maisha. Watoto wengine wawili wa Babu Seya, waliokuwemo kwenye kesi hiyo ni Francis Nguza na Nguza Mbangu ‘Nguza Mashine’ aliyekuwa mpiga drum wa Bendi ya FM Academia, mpaka wakati anaingizwa kwenye mashtaka. Mwaka 2005, rufaa ya kwanza ilisomwa ambayo ilikazia hukumu ya awali lakini Februari 2010, Mbangu na Francis waliachiwa huru baada ya kuonekana hawana hatia, huku Babu Seya na Papii, ikipitishwa na Mahakama ya Rufaa kwamba waendelee na kifungo cha maisha jela. MAJAJI WALIVYOTOA HUKUMU Zahra, alisema jopo la majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Masati na Mbarouk Salim Mbarouk, lilichambua hoja za utetezi na kuona hazina nguvu, kwa hiyo wakajiridhisha kuwa Babu Seya na Papii, wanastahili kuendelea na adhabu ya kifungo cha maisha jela. Hukumu hiyo, ilikuwa ni ya rufaa ya nne, lakini imeshindikana kwa kuwaondoa Babu Seya kwenye kifungo. MAWAKILI WASALIMU AMRI Mmoja wa  mawakili wa utetezi, Mjele, alisema kuwa hukumu hiyo ndiyo ya mwisho na kwamba wao hawana njia nyingine ya kukata rufaa kisheria. “Hatuna njia nyingine, hapa ndiyo mwisho,” alisema Mjele na kuongeza: “Labda tusubiri msamaha wa rais kwa sababu ni yeye pekee mwenye mamlaka ya kutengua hii adhabu.” RAIS AZIDI KUTUPIWA MZIGO Watu kadhaa waliohudhuria mahakamani juzi, waliungana na Wakili Mjele kwamba kesi hiyo iachwe mikononi mwa rais kwa sababu ndiye mwenye nafasi ya kufanya lolote katika kesi hiyo kama anavyoruhusiwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Mahakama imefanya kazi yake, mawakili wa utetezi wamejitahidi lakini imeshindikana, sasa hatutakiwi kuijadili sana hukumu, badala yake tumuachie rais kwa sababu ndiye mwenye mamlaka,” alisema Fredrick Mwaluwanda wa Kinyerezi. Mosha Kabogo alisema: “Katika hukumu hii, kila mmoja anaweza kuwa na hisia zake, jambo la msingi ni kumuacha rais afanye anachoona kinafaa. Uzuri ni kwamba siyo rais wa sasa peke yake, kwani hata ye yote anayekuja, anaweza kutumia mamlaka yake kikatiba kuwaachia huru au kuwapunguzia adhabu.” WANAMUZIKI WAANDAA UJUMBE KWA RAIS Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, alisema mahakamani hapo kuwa anakusudia kuitisha kongamano la wanamuziki halafu watafanya mkutano na waandishi wa habari kumuomba rais awaachie huru Babu Seya na Papii. “Hili suala linauma sana, hatuwezi kukaa kimya tukiwaacha wanamuziki wetu nyota wakienda na maji. Lazima tufanye kitu na tutakachofanya  ni kujikusanya na kuandaa mkutano wa waandishi wa habari ambao tutautumia kutuma ujumbe kwa mheshimiwa rais,” alisema Dully. PAPII NI WA KUMJADILI KIDOGO Papii Kocha, wakati alipoingia kwenye mashtaka hayo, alikuwa ni kijana mdogo ambaye nyota yake kwenye muziki ilikuwa inang’ara kwa kiwango cha juu sana nchini Tanzania. Alifanya vizuri sana akiwa na Bendi ya FM Academia na Tot Plus kabla ya kutoka na albamu yake binafsi iliyokuwa na nyimbo nyingi kama vile Salima, Fanta na Seya ambayo uliimbwa mithili ya wimbo wa taifa. Alitabiriwa kwamba angeweza kuendelea kufanya vizuri kutokana na uwezo aliokuwa nao lakini nyota yake ilizimwa na kesi hiyo. Kwa upande wa Babu Seya, ni nguli aliyejenga jina na heshima kubwa nchini kupitia muziki wake, huku akipigiwa mfano kama mpiga solo bora kabisa, lakini historia yake imehitimishwa kwa kifungo cha maisha jela. HABARI NA PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS Previous Article Next Article RAGE AWASILI KISHUJAA, MAMIA WAMLAKI UWANJA NDEGE, ASEMA YEYE BADO MWENYEKITI SIMBA, HANS POPPE NAYE… November 22, 2013, 7:25 pm Ahaj Ismail Aden Rage Na Mahmoud Zubeiry, JNIA MWENYEKITI wa Simba SC, Ahaj Ismail Aden Rage amewasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam usiku huu akitokea Sudan na kusema kwamba; “Mimi bado Mwenyekiti wa Simba SC,”. Rage aliwasili kwa ndege ya shirika la Kenya saa 1:40 usiku wa kuamkia leo na kutokea mlango wa Watu maalum (VIP) ambako alilakiwa na wanachama zaidi ya 200, waliokuwa kwenye mabasi sita aina ya Coaster. “Umati huu uliokuja hapa ni kielelezo tosha sana kwamba kiasi gani wanachama wa Simba wana imani na Mwenyekiti wao, sasa leo sitasema mengi, nitakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari kesho saa saba mchana makao makuu ya klabu(Msimbazi),”alisema Rage. Rage akiinua mikono juu kishujaa wakati anatoka Uwanja wa Julius Nyerere, Dar es Salaam usiku wa leo Alipoulizwa kuhusu kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Jumatatu na kutangaza kumsimamisha, Rage alisema; “Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Kamati ya Utendaji haina uwezo wa kumsimamisha Mwenyekiti, usinimalizie utamu Zubeiry, njoo kesho mchana Msimbazi,”alisema. Watu zaidi ya 200 walifika Uwanja wa ndege tangu saa 11 na ushei jioni ya leo kumsubiri Rage wakiimba nyimbo mbalimbali za kumbeza Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na kumpamba Rage huku wakicheza ngoma. Na alipowasili walimlaki kwa shangwe na kucheza naye. Ilikuwa bonge la picha na waliofika kumlaki Rage walikuwa watu wa rika na jinsia tofauti, hadi wazee. Rage baada ya kuzungumza kwa kifupi na Waandishi wa Habari alisema anaelekea makao makuu ya klabu, ambako wanachama wengine walikuwa huko wanamsubiri. Jumanne wiki hii, Kinesi alisema, Kamati ya Utendaji ilimsimamisha Rage katika kikao chake cha Jumatatu usiku kwa sababu anaendesha klabu kwa kufanya maamuzi yake mwenyewe bila kushirikisha kamati ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (a). Alisema sababu nyingine ni Rage kuahirisha mkutano Mkuu maalum wa katiba ulioidhinishwa na mkutano mkuu bila kuishirikisha kamati. “Rage alisema mkutano usifanyike kwa sababu alikuwa na safari ya nje na kutaka matawi yaendelee kuleta taarifa za katiba, sisi tukaona kikatiba mkutano lazima uendelee kwani alikaidi,”alisema Kinesi. Aidha, sababu nyingine ni mkataba wa kukiuza kipindi cha Simba Tv bila kuishirikisha kamati hiyo kinyume na ibara ya 30 (b) ya ibara ya katiba ilihali kamati hiyo na Mwenyekiti akiwa na taarifa ilikuwa na mazungumzo na Zuku Tv, kuuza kipindi hicho ambapo maongezi yalikuwa yamefikia Dola za Marekani 300,000 kwa mwaka pamoja na fungu la usajili kila mwaka ambalo lilikuwa bado halijajadiliwa. Hata hivyo, Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, limesema halitambui uamuzi huo wa Kamati ya Utendaji na kumuandikia barua Kinesi aliyeendesha kikao hicho kumtaka awape muhtasari wa kikao na pia aeleze wajumbe waliohudhuria. Msinipokeel msubirini Rage; Hans Poppe akiwasili JNIA Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Simba, Hamisi Kilomoni, alisema ingawa baraza bado halijajulishwa rasmi uamuzi wa kumsimamisha Rage, lakini wamekubaliana kwamba kuna makosa yalifanyika kwenye kikao hicho kulingana na katiba ya Simba, hivyo kutaka muhtasari huo kwa vile wao ndiyo wasimamizi wa masuala ya Simba. “Kwanza mimi na mwenzangu Ramesh Patel (Mjumbe wa Baraza la Wadhamini) tumekubaliana kuna makosa yalifanyika kwenye kikao chao, hivyo uamuzi wao si sahihi. Tulichokifanya tumemuandikia barua Mwenyekiti aliyesimamia hicho kikao, atupe muhtasari wa kilichotokea na pia tufahamu wajumbe waliohudhuria. “Sisi hawajatujulisha rasmi, badala yake nasi tumepata taarifa kutokana na vyombo vya habari, na kama unavyojua inawezekana kwenye vyombo vya habari kuna taarifa tofauti na yaliyojitokeza kwenye kikao… “Hivyo ndiyo sababu tunataka muhtsari wa kikao ili kwanza tupate uhakika wa mambo, tujue walizungumza nini na masuala kama hayo. Ila kama walijadili kama yanavyoelezwa kwenye magazeti, wamefanya makosa. Katiba haisemi hivyo, ” alisema Kilomoni ambaye amepata kuwa kiongozi wa Simba na pia mchezaji wa timu hiyo. Wakati huo huo: Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe naye amewasili leo ndege moja na Rage, ingawa yeye ametokea, Lubumbashi, DRC alipokwenda kwa shughuli zake za kibiashara. Hans Poppe, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) aliwavutia wanachama wa Simba SC alipotokea, lakini akawaomba hataki mapokezi, waendelee kumsubiri Rage. “Msinipokee tafadhali, nawashukuru, msubirini Rage anakuja huko nyuma, nimemuacha ndani,”alisema. Hans Poppe ni kipenzi cha wapenzi na wanachama wa Simba SC kutokana mchango wake mkubwa anautoa kwenye klabu hiyo wa hali na mali. Previous Article Next Article PROF. BAREGU NAYE PIA AJIUZULU CHADEMA November 22, 2013, 7:34 pm Mjumbe wa tume ya mabadiliko ya Katiba kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ametoa kauli ya kujiondoa na kujiuzulu nafasi zake ndani ya Chama hicho kupelekea maamuzi yaliyofanywa na kikao cha kamati kuu ya chama hicho Huyu ni Mjumbe wa pili wa kamati kuu ya Chadema kuamua kujiuzulu wadhifa wake katika kipindi kisichozidi masaa 12. Previous Article Next Article EADERS:LADY JAYDEE AKIFANYA YAKE STEJINI USIKU WA KUAMKIA LEO November 23, 2013, 8:00 pm Mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee' au 'Anaconda' akiwapagawisha mashabiki wake waliohudhuria katika Viwanja vya Leaders  katika shoo wa wakali P-Square. Watu... Jideeeeeeeeeeee... Machozi Band nao walikuwepo kumback up Jide. (PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL) Previous Article Next Article LEADERS CLUB:PROFESA JAY AWADATISHA MASHABIKI November 23, 2013, 8:05 pm Mwanamuziki Joseph Haule 'Profesa Jay' akiwapagawisha vilivyo mashabiki waliohudhuria shoo ya P-Square Live in Dar ndani ya Viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar. Nyomi baada ya kuikubali vilivyo shoo ya Profesa Jay. (PICHA NA MUSA MATEJA / GPL) Previous Article Next Article P-SQUARE LIVE IN DAR November 23, 2013, 8:08 pm Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square wakilivamia jukwaa la Leaders. Mashabiki wakipagawa na shoo ya P-Square. Joh Makini akilitawala jukwaa. Nikki wa Pili (kushoto) na G Nako wakifanya yao stejini. Kundi la Weusi likiongozwa na Joh Makini likishambulia jukwaa la Leaders Club. (PICHA NA MUSA MATEJA /GPL) Previous Article Next Article ZITTO KABWE NA DKT. KITILA MKUMBO WAFUNGUKA November 25, 2013, 1:48 am Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,wakati akitoa taarifa yake ya kuhusu kuvuliwa nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo (kushoto),kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo akizungumza. Zitto Kabwe (kulia) na Dk. Kitilla Mkumbo, wakisikiliza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo. Sehemu ya Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali wakiwa kwenye Mkutano huo,uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam leo. Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo wakiingia Ukumbini katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari. Zitto Kabwe, akiagana na baadhi ya waandishi wa habari wakati akiondoka ukumbini. Na Ripota wetu, Dar es Salaam. MBUNGE wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe amesema hawezi kufanya maamuzi magumu ya kutaka kujitoa ndani ya chama hicho kwa kile kilichotokea ndani ya chama hicho hivi karibuni. Amesema yeye atakuwa wa mwisho kutoka Chadema na si vinginevyo,kama wanavyofikiria watu wengine. Zitto ameyatoa maneno hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,wakati alikizungumzia maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema ya kumvua nafasi zake zote za uongozi yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Dk. Kitilla Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa  Arusha,Samson Mwigamba. Zitto amekana kabisa kuhusika na wala kuujua waraka wa siri ambao ndiyo uliosababisha kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama kuunasa waraka huo. "Mimi nimeusikia ule waraka kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu na nilisikitika sana kwanini haukunifikia haraka kwani ningeanza kutekeleza mara moja." alisema Zitto akizungumza. Zitto aliendelea kusema "Huenda leo watu walitegemea nitafanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye chama; "Mimi bado ni mwanachama wa Chadema na nitakaekuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiyari yangu, nitafanya taratibu zote za chama kuhitimisha jambo hili mimi sitoki ng'o kwenye chama hiki labda wanitoe wao," alisema Zitto. Zitto alisema anaumia sana anapotuhumiwa kwa kuwa yeye ni binadamu. "...ninapotuhumiwa naumia ninapoambiwa nahujumu chama hiki naumia kwa kuwa nakipenda chama na nimekitumikia muda mrefu. Aidha aliwataka viongozi wa Chadema kuacha siasa za uzushi ili kujenga chama imara na kuwakomboa Watanzania. "...Sisemi kama mimi sina makosa,kwani mimi ni binadamu na nimefanya mambo mengi kwa chama changu, lakini kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia na ni mapambano ya wanaotaka mabadiliko na wasiopenda mabadiliko ndani ya chama...mapambano ya wawajibikaji na wasiopenda kuwajibika ni mapambano ya wanaopenda demokrasia na wanaokwaza demokrasia." alisema Zitto huku akionesha kusikitishwa. TAARIFA YA MH. ZITTO KABWE Previous Article Next Article RAGE AMGOMEA MALINZI, ASEMA HAKUNA MKUTANO SIMBA November 25, 2013, 2:05 am MWENYEKITI wa Simba Ismail Aden Rage amesikia taarifa aliyotumiwa na Shirikisho la Tanzania (TFF) la kumtaka kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa klabu hiyo. Rage ametangaza msimamo wake huo siku ya jana ambapo amesema kamwe hawezi kuafiki kuchukua uamuzi huo kutokana na TFF kuingilia majukumu yake. Rage amesema katiba ya Simba ibara ya 22 inaeleza wazi kwamba mwenyekiti akishirikiana na kamati yake ya utendaji wanaweza kuitisha mkutano mkuu wa dharura kama wataona kuna haja ya kufanya hivyo. Amesema hakufurahishwa na uamuzi huo wa TFF ambapo alitegemea kwanza shirikisho hilo kupitia kamati yake ya utendaji inayoongozwa na Rais Jamal Malinzi lingekemea mapinduzi aliyofanyiwa. “Katiba inatamka wazi mwenye mamlaka ya kuitisha mkutano mkuu ninayo mimi nikishirikiana na kamati ya utendaji na kwa jinsi hali ilivyo sioni haja ya kufanya hivyo, nasema hakuna mkutano,” alisema Rage. Aidha Rage amesema endapo TFF itaendelea kumlazimisha kufanya hivyo hatasita kuchukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yake hiyo. Previous Article Next Article Malkia wa nyuki aandika barua kujitoa Simba November 25, 2013, 2:17 am MALKIA wa Nyuki ameandika barua ya kujiondoa kwenye Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba kutokana na kuchukizwa na migogoro. Malkia ambaye jina lake halisi ni Rahma Al Kharusi, amethibitisha hilo na kusema aliamua kufanya hivyo kutokana na kukerwa na migogoro ndani ya kamati hiyo. Akizungumza jana kutoka Oman, Malkia wa Nyuki alisema aliamua kujiondoa kwa mambo mawili makubwa ambayo ni migogoro na kukosa nafasi. “Baada ya kumueleza Rage kwamba nimefikia uamuzi huo, ameniomba nibaki kwa kuwa ninahitajika Simba. Kanishauri kwamba niingie katika upande wa baraza la wadhamini. Kwangu naona si mbaya, maana sitakuwa na vikao vya mara kwa mara, lakini bado nasisitiza migogoro si sahihi,” alisema. “Kwani kama si kuteuliwa katika nafasi hii ya kusimamia mali za Simba, basi nilikuwa nimeshajiondoa kabisa Simba hadi hapo hali itulie maana sioni faida ya haya yaliyopo sasa.” Malkia wa Nyuki, ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Simba, ndiye alitoa zaidi ya Sh milioni 80, Simba ikaweka kambi ya siku 15 jijini Muscat nchini Oman. Lakini aliahidi kuanza kushughulikia kujenga uwanja kwa ajili ya mazoezi, pia alifunga safari kwenda kufanya mazungumzo na Sunderland kuisaidia Simba, lakini amekuwa akilalama kwamba migogoro na utendaji mbovu ni tatizo. Katika mkutano wa jana jijini Dar, Rage alitangaza kumteua Malkia katika nafasi hiyo na nafasi yake katika kamati ya utendaji akamteua Michael Richard Wambura aliyewahi kuwa katibu mkuu Simba. Previous Article Next Article Rage awapanga mashabiki wamshangilie November 25, 2013, 2:21 am KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Rage, amewapanga mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa ajili ya kumshangilia. Tukio hilo la aina yake lilifanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Msimbazi jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari, jana. Mwenyekiti huyo akisubiriwa na kundi kubwa la mashabiki hao nje ya ofisi hiyo ya Simba, alionekana na kusikika akiwapanga kwa ajili ya kumshangilia. Rage alimuita pembeni mmoja wa makomandoo wa klabu hiyo na kumtaka ashuke kutoka ghorofani haraka na kwenda kuwaambia mashabiki wajiandae kwa ajili ya kumshangilia akiwa anatoka mjengoni hapo. Mwenyekiti huyo alisikika akiwaambia waandishi wa habari: “Mnataka mnione nikiwa nashangiliwa na mashabiki, basi subirini muone nitakavyoshangiliwa. “Anzeni nyie waandishi wa habari kuanza kushuka chini mkiwa na kamera zenu muone nitakavyoshangiliwa, ndiyo muamini kuwa napendwa.” Waandishi bila kujali, haraka wakashuka chini na kukuta kundi la mashabiki waliokuwa wanamsubiri mwenyekiti kwa shauku kubwa kwa ajili ya kumshangilia. Mara baada ya kushuka chini alipokewa na mashabiki hao kwa shangwe kwa kumpa mikono na wengine kumnyooshea wakimpongeza na kumtaka aendelee kukaa madarakani. Aliposhuka chini alisimama kama dakika tano kwa ajili ya kuzungumza na mashabiki hao na baadaye kuelekea kwenye gari aina ya Toyota V6 Granvia lenye namba T 300 CPR. Baada ya kuingia kwenye gari alifungua dirisha la juu la gari hilo na kusimama na kuwapungia mikono mashabiki hao wachache ambao walikuwa wakiimba Simba! Simba! Simba! Simbaaa! Kwa sauti kali hadi gari hilo lilipoondoka likisukumwa na kundi hilo. Previous Article Next Article KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI WILAYANI RUNGWE‏ November 25, 2013, 2:23 am 1 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Bw. Crispin Meela katika mji wa Ushirika wilayani Rungwe mara baada ya kuwasili wilayani huo, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya ambayo aliianza jana wilayani Kyela akitokea Mbamba Bay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma , Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa , Kinana ameanza kazi katika wilaya ya Rungwe kwa kufanya mkutano wa ndani ambapo atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na uhai wa chama wilayani huo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUNGWE 2 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki Mh. David Mwakyusa mara baada ya kuwasili katika mji wa Ushirika Wilayani Rungwe ambapo ndipo alipopokelewa leo 3 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Richard Kasesela mmoja wa wana CCM waliofika kwenye mapokezi hayo. 5 Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akisalimiana na Richard Kasesela katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Nd. Crispin Meela. 6 Baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Rungwe wakiwa katika mkutano wa ndani ambao Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri mjini Tukuyu. 7 Baadhi ya wajumbe wakimpokea Ndugu Abdulrahman Kinana tayari kwa kikao hicho cha ndani. 8 Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh Godfrey Zambi ,Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakisaini vitabu vya wageni mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano mjini Tukuyu. Previous Article Next Article HYATT REGENCY KILIMANJARO HOTEL SET ASIDE USD 50,000 FOR CSR‏ November 25, 2013, 4:20 am DSC_0022 Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel General Manager Trevor Saldanha speaks to invited guests during the business partner celebrations hosted by The Kilimanjaro Hotel to his customers in Dar es Salaam. By MOblog Team HYATT Regency the Kilimanjaro Hotel has set aside USD 50,000 as part of the hotel’s Corporate Social Responsibility (CSR) efforts to foster the development of education sector in the country. It has been learnt. Speaking to invited dignitaries during the dinner party hosted by the Kilimanjaro hotel to its customers yesterday in Dar es Salaam, General Manager Trevor Saldanha said the funds would be used to repair and rehabilitate Mtoni Primary school in the Temeke municipality. “Equally important when in business is to give back to the community one operates in and I would like to mention here that “The Kilimanjaro” as part of its corporate social responsibility has kept aside 50,000 dollars that is being used to repair & maintain the Mtoni School,” “ We have already begun working with the school principal on the areas that are in urgent need of repair and while some work is being done with the help of outside contractors a lot of this project is being completed with the help of hotel employees who donate their free time to this important cause,” “We are also partnering with His Worship The Lord Mayor of Ilala, Jerry Silaa on his project for 2013 which is to ensure that every child attending a public school has a bench to sit on,” says Saldanha He said that the hotel will always remain the iconic “Kilimanjaro Hotel”; all team members will work hard to live up to the name and represent the brand to the best of theory collective abilities. Saldanha added that the hotel continues to be the preferred residence of Kings, Queens, Presidents, Prime Ministers, Entrepreneurs and Entertainers when they visit Dar es Salaam (some of you may have already caught a glimpse of some of our famous guests on the screens). He further said that the aim of any company is to expand and increase its enterprise value and Hyatt is currently constructing a 77 room hotel in historic Stone Town, Hyatt will commission the new “Park Hyatt Zanzibar” next year. This spectacular property will set the tone for hospitality on the island. DSC_0088 Mr.Timoth Mlay The Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel, Front Office Manager along side with Sam Sarin Sales Executive Manager conducting a draw where by invited guests wins various Hampers. DSC_0135 Sam Sarin Sales Executive Manager of the Kilimanjaro Hotel display a bottle of Hennessey from Q Way International. DSC_0532 An Employee from Commercial Bank of Africa (CBA) Rehema Mashayo in a happy mood when she was announced as a lucky winner of the Business Class return Ticket from Dar to Instanbul when Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel conducted a draw on behalf of Turkish Airline. DSC_0533 Turkish Airlines Director, Tanzania Alper KUCUK congratulate Ms. Rehema Mashayo from CBA Bank for being one of the lucky winners during Business Partners celebrations hosted by The Kilimanjaro Hotel Hyatt Regency. DSC_0535 Turkish Airlines Director, Tanzania Alper KUCUK hands over an example of the return ticket Ms. Rehema Mashayo from CBA Bank. DSC_0556 Turkish Airlines Director, Tanzania Alper KUCUK display an example of the returning ticket of Ms.Rehema Mashayo. DSC_0247 His worship Lord Mayor Hon. Jerry Silaa shares a light moment with Jacqueline Kombe (left) from High Commissioner of Canada and Jully Urio (right) during the Business Partner Celebrations hosted by The Kilimanjaro Hyatt Regency Hotel. For more pictures click here Previous Article Next Article Zitto ajiweka njia panda November 26, 2013, 1:55 am Dar es Salaam. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amejiweka katika mazingira magumu zaidi kisiasa ndani ya chama hicho, kutokana na shaka kubwa iliyougubika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam juzi. Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani. Leo, uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM). Miongoni mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa nyadhifa zao. Mchange na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM wanakoendeleza harakati zao za kisiasa. Jana, Machange alipotafutwa, alisema: “Mimi sikuwahi kuondoka Chadema, nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema nimeondoka. Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu. “Mimi ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote, walioondoka ni Mwampamba na Shonza.” Mwampamba alisema: “Nilijitokeza pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu.” Kuwepo kwao katika mkutano wa Zitto kunaweza kutumiwa na uongozi wa Chadema kuwa uthibitisho wa kiongozi huyo kushiriki katika uasi na kunaweza kupuunguzia nguvu utetezi unaotolewa na Dk Kitila kwamba hakuwa sehemu mpango wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani. Zitto, Dk Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba wanasubiri kukabidhiwa barua za kuvuliwa kwao madaraka na katika siku 14 wanapaswa wawe wamewasilisha utetezi wao wakieleza kwa nini wasifukuzwe uanachama kutokana na tuhuma zinazowakabili. Dk Slaa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema jana kuwa ilikuwa lazima viongozi hao wavuliwe madaraka hasa baada ya Dk Kitila kukiri kuhusika na waraka ambao anasema ulilenga kushinda kupitia uchaguzi halali ndani ya chama hicho. “Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?” alihoji Dk Slaa.Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: “Wao nani kawaambia waende kwa waandishi wa habari?” “Mimi ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?” alihoji Dk Slaa. Mkutano leo Mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu  baadhi ya hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu. Habari zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni “Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu”, badala ya kujibu hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu. Jana, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa tuhuma za kusema na za kuacha... “Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya hivyo?” Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: “Kamati Kuu ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu kama chama.” Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda uongozi wa Chadema ukaweka wazi “makosa mengine” ambayo Zitto anadaiwa kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi ya miezi sita. “Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati Kuu imechoka,” alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu. Habari zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi ndiyo inapaswa kuiandaa. Wasomi wanena Akizungumzia mgogoro huo, mtaalamu wa mambo ya siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hali inayoendelea ndani ya Chadema ni matokeo ya vyama vya siasa kutofanya kazi kama taasisi. “Misingi ya vyama haiweki wazi misingi ya watu kuwa viongozi. Kwa mfano, kesho nikitaka kujiunga na Chadema nitaweza kuwa Mwenyekiti? Misingi ya wazi hakuna,” alisema Mbunda. Alisema hali ilivyo ndani ya Chadema kwa sasa ni furaha ndani ya CCM, kwani watu wanaona kuwa chama kilichoonekana kuwa mbadala hakiwezi hata kushughulikia mambo yake ya ndani. Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema vyama vya siasa ni watu au kikundi cha watu wenye malengo na mitazamo tofauti. “Ukisoma huo waraka utaona kuwa unazungumzia uongozi, upungufu uliopo kwenye uongozi na namna ya kubadili uongozi, mimi binafsi niseme ieleweke kwamba hata kwenye jumuiya yoyote mambo haya yapo hasa kwa kuwa walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi,” alisema. Alisema haoni kwa nini Zitto na Dk Kitila waonekane wahaini kwa kupanga mikakati yao ambayo walitaka kuitekeleza kupitia uchaguzi. “Mabadiliko ni jambo la kawaida, hali hii ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao inawezekana ikawagharimu Chadema na inaweza kuwagharimu zaidi wakiwafukuza uanachama,” alisema Makulilo. CREDIT:MWANANCHI Previous Article Next Article Taarifa Maalum Kutoka Chadema Kwa Umma kuhusu Mch.Israel Natse, Peter Msingwa na Profesa Mwesiga Baregu November 26, 2013, 1:59 am Tangu kumalizika kwa vikao vya Kamati Kuu ya CHADEMA, iliyoketi kwa siku mbili mfululizo Novemba 20-21, mwaka huu, kisha maazimio yake kutolewa kwa wanachama na umma wa Watanzania siku ya jana, kumeanza kuibuliwa propaganda nyingi zenye makusudi maalum. Ni wazi kuwa hatuwezi kukimbizana na wapika propanda (rumourville is back?), kwa kujibizana nao kwa kila wanachokisema. Itakuwa ni kufanya kazi wanazotaka wao tufanye badala ya kuendelea kutekeleza majukumu ya kuimarisha taasisi na mifumo, hasa katika wakati huu ambapo CHADEMA inaendelea kutimiza wajibu mkubwa kwa wanachama wake na Watanzania wote kwa ujumla. Pamoja na kwamba propaganda hizo nyingi zinapuuzwa, si kila upuuzi unaweza kupuuzwa. Mathalani zimeenezwa habari zauongo kuwa Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse amekuwa Makamu Mwenyekiti Bara, Mbunge wa Iringa Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu, Peter Msigwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Prof. Mwesiga Baregu, amejiuzulu nafasi yake ya ujumbe wa Kamati Kuu. Kwa mtu makini, ukisikia na kuzisoma propaganda hizo katikati ya maneno kama si mistari, mara moja unang'amua zinalenga kitu gani. Kwa sasa si lazima kuingia undani wa malengo hayo, lakini ni vyema ikajulikana kuwa yanajulikana tayari. Hazitafuzu. Tunatambua kuwepo kwa watu wa CCM, wakiwemo viongozi wa juu kabisa wa chama hicho, wanaoonekana eti 'wanaipenda' CHADEMA leo ghafla, wanahusika katika kueneza uongo na propaganda hizo. Bila shaka ni dalili ya kushindwa kushughulika na mambo yao (ufisadi, kujivua gamba, kukataliwa na wananchi, n.k), kiasi wanapata muda wa 'kujali' ya wengine. Tunajua wanatishika na namna ambavyo CHADEMA inaendelea kujiimarisha (huku wao wakizidi kukataliwa), kupitia CHADEMA ni msingi na Operesheni ya M4C, kupitia kanda za chama na kazi nyingine zinazeondelea yakiwemo mafunzo kwa viongozi. Wanachama makini wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanaoamini kwa dhati katika mapambano ya mabadiliko ambayo chama hiki kimeyasimamia consistently, bila kuyumba, kikionesha kila sifa ya kuwa mbadala wa status quo ya CCM, wataendelea kusikiliza chama chao kinasema nini (hasa kupitia maamuzi ya vikao), kuhakikisha nguvu ya mshikamano wa pamoja inaendelea kuwa ndiyo nguzo imara ya mafanikio kwa ajili ya haki nha matumaini ya Watanzania. Propaganda za hivi sasa, kama ambavyo zimeshindwa zote zingine, hazitawaondoa katika mstari wanachama na Watanzania wenye matumaini makubwa na CHADEMA kuwa ni chama mbadala chenye kujenga uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganaizesehni tahibiti, mijini na vijijini kwa ajili ya kutoa utumishi bora kwa wananchi. Imetolewa na:- Tumaini Makene Msemaji wa CHADEMA 0752 691569 22 Novemba 2013 Previous Article Next Article JUMUIYA YA WANA-MASOKO YA WANAFUNZI WA CBE WAANDAA MHADHARA WA WAZI‏ November 26, 2013, 2:19 am Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE)wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa(hayupo pichani) ambae ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa kwenye mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuoni hapo. Naibu Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Dr. Abby Nangawe akiongea muda mfupi kabla ya kuanza kwa mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuo hicho.Katika ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa ambae ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa kwenye mhadhara huo na kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa CBE Godian Bwemelo.Mhadhara huo ulifanyika jana chuoni hapo jijini Dra es salaam. Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akizungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana. Twissa alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mdahalo wa wazi chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta ya masoko na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobebea katika fani  mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi. Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akionesha kwa vitendo mbinu za kimasoko Wakati alipoalikwa kuzungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana. Twissa ni mmoja kati ya vijana waliobobea katika Nyanja ya masoko na matangazo nchini na alialikwa chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta hizo na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobebea katika fani  mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi. Previous Article Next Article ZITTO AICHANGANYA CHADEMA,WATANGAZA UCHAGUZI MKUU November 26, 2013, 5:34 am WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikipinga waraka uliosambazwa kwenye vyonbo vya habari na katika mitandao mbalimbali kuwa ni feki ila walionao ndiyo orijino,Chama hicho leo hii kimetangaza mchakato wa kuanza kwa Uchaguzi Mkuu wa ndani, kuanzia balozi wa nyumba kumi hadi ngazi ya Mwenyekiti wa Chama Kitaifa. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu amesema kwamba mchakato wa uchaguzi huo uta anza rasmi January mwaka 2014 na kukamilika Juni.Hatua ya Chadema kutangaza kuanza kwa uchaguzi huo ni sawa na kujibu hoja iliyokuwa katika waraka uliosababisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama Zitto Kabwe na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Dk Kitilia Mkumbo kuvuliwa nyadhifa zao zote ndani ya Chama. Mwanasheria Mkuu wa Chadema,Tundu Lissu akionyesha waraka aliodai kuwa ni orijino badala ya ule uliosambazwa kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari aliodai kuwa ni feki,kushoto ni John Mnyika na Mbunge wa Ubungo na Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi Wilfred Lwakatare. Kwa muujibu wa waraka huo ambayo Lissu amesema kwamba ni feki wahusika walidai kwmaba lengo la kwanza ilikuwa ni kuandaa mpango mkakati wa kuilazimisha Chama hicho kufanya Uchaguzi Mkuu kutokana na viongozi wake kukwepa uchaguzi huo mara kwa mara. Katika hatua nyingine Zitto na Mwenzake Dk Kitilia wamepewa hati ya mashtaka ya tuhuma zao yenye tuhuma 11 kila mmoja, ambazo wanatakiwa kuyajibu kwa maandishi ndani ya siku 14 kabla ya kuitwa katika Kamati Kuu kwa kujieleza kabla ya maamuzi ya ama wafukuzwe ama wasifukuzwe kufanyika.Ndugu mdau wa tovuti ya Habarimpya.com,endelea kutembelea tovuti yetu,kwa habari zaidi. Previous Article Next Article SHARO MILIONEA ATIMIZA MWAKA TANGU ALIPOFARIKI November 26, 2013, 7:39 am Marehemu Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’( 1985 - 2012 ) enzi za uhai wake. Hili ndio Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga. Marehemu Sharo Milionea alifariki dunia tarehe 26 Novemba , 2012 kwa ajali mbaya ya Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR wakati akitoa Dar es Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga.Alipofika maeneo ya maguzoni nje kidogo na wilayani Muheza gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti na kusababisha kifo chake na yeye kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali. Previous Article Next Article VIJANA WAJIRUSHA BAHARINI KUTOKA JUU YA PANTONI KWENYE KIVUKO CHA KIGAMBONI November 27, 2013, 4:54 am Katika hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushangaza, kumemezuka tabia ya vijana ambao wanashinda kakika kivuko kinacho unganisha Posta na Kigamboni wakivizia kivuko hicho kinapopita kupanda na baadae kinapo ondoka hata kikifika umbali mrefu wao kuanza kuruka na kupiga mbizi. Mtandao huu wa Dar es salaam yetu umekuwa ukifuatilia kwa kina swala hili na kigundua kuwa hakuna mtu ambaye anawazuia vijana hawa wanaofanya mchezo wa hatari, ingawa kwa upande wa pili kimekuwa ni kivutio kikubwa kwa wale wasafiri.. Vijana hawa ambao hawalipii hata kiasi kidogo katika kivuko hicho wameendelea kuhatarisha maisha yao na pindi wakijua na kufahamu kabisa eneo ambalo kivuko kinapita huwa ni sehemu ndefu sana ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwao na pengine kifo. Hata hivyo inawezekana wahusika hawalijui hili au lah wanalijua lakini hawalizuii, hili ni jambo letu sote kujiuliza. Tazama sasa hapa kinacho tokea..... Pichani ni Kijana ambaye alionekana anaruka kutoka Juu ya Pantoni(Kivuko) Mbele kidogo baada ya Pantoni hiyo MV. Magogoni kuanza safari zake, huku abiria wengi wakiwa wameacha viti vyao na kuendelea kushangaa. Wakati huo huo Kijana mwengine nae alionekana anachomokea kutoka katika Pantoni hiyo na kuzamia majini Wasafiri walipigwa Butwaa zaidi kuona kasi ya vijana hao inazidi kuongezeka na huyu kijanda ndiye aliyekuwa anafunga dimba la kuzamia majini. Hapa ni Baada ya vijana hao kuzamia majini na wengine hawaonekani yanaonekana maji tuu yanaruka wakati wao wapo chini ya maji hayo. Ni zaidi ya Vijana 9 ambao wote walipanda Pantoni hiyo ya MV.MAGOGONI bila ulinzi wowote na baadae kupiga Mbizi wakitokea katika Pantoni hilo... Picha zote na Dar es salaam yetu Blog

Blog