Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

LIMBWATA

 



MTUNZI : GEOFREY MALWA


Wanaume! Wanaume!
Hivi ni nini lilikuwa kusudio la kuumbwa kwao?
Wengi wao wamekuwa wajinga na watumwa wa kupenda chini, eeh..chini, tena hilo wala halina ubishi. Chini kumeua wengi japo kumetoa wengi, nathubutu kusema, hakuna mwanaume duniani anayeweza kuridhika na mwanamke mmoja.

Maisha yangu kabla ya kuolewa yalikuwa ya maumivu na raha kwa nyakati tofauti, nilishawahi kuwatenda wanaume kadhaa, lakini pia nilishawahi kutendwa. Sikuwahi kuchukulia mahusiano ‘siriazi’ sana hali iliyowafanya wanaume nilioishi nao kuniona nina dharau na maringo.

Debora ndilo lilikuwa jina langu, mwanamke mwenye uzuri wa kipekee, laiti kama ungeulizwa kwamba nilikuwa mnene au mwembamba, ungepata kugugumizi cha kujibu, wastani ndilo jibu ambalo ungelitoa. Nilijaaliwa urefu wa wastani, umbo lililojaa uchokozi wa kumwamsha jogoo wa kidume yeyote. Ukishachemsha kunde, yale maji yake ndio yalifanana na rangi yangu ya mwili. Sikusubiri kuambiwa, nilikuwa mzuri tena sio mzuri tu, mwenye ushawishi mkubwa kwa wanaume wengi.

Muda ulimleta mwanaume niliyempenda, aliitwa Didasi, sikuwahi kuhisi wivu kwa mwanaume lakini kwake ilikuwa tofauti. Yeye pia alinipenda sana, kutokana na uzuri wangu alikuwa akinitilia mashaka kuniweka karibu muda wote. Alipolileta suala la ndoa mezani, sikulipinga japo tuliishi kwa muda wa miezi mitatu tu. Kusema kweli sikumjua sana undani wake, ila upendo uliniongoza, pia uhakika wa maisha ulinivuta, alimiliki nyumba ya kisasa na gari la kutembelea.

Ndoa ikapita, maisha mapya yakaanza, uwanja wangu ulikuwa ukitifuliwa vya kutosha, kila nilipokuwa nikipita mtandaoni na kuona matangazo ya dawa nyingi za kumnenepesha au kumrefusha jogoo, mara kumfanya jogoo awike kwa muda mrefu bila kusinzia, kwangu niliona kama kelele tu kwani babaa akiliamsha unaweza ukaomba poo wakati hamchezi mchezo wa kidali poo.

Nikajisemea mwanamke ndio mimi, uzuri wangu ulitendewa haki, kama ni gari nililikabidhi mikononi mwa mwalimu wa madereva. Didasi alikuwa akifanya biashara ya kuuza komputa za aina zote, vifaa vingi vya kielektroniki, friji, runinga za kisasa, ving’amuzi na vinginevyo vingi.

Hata mwaka hatukumaliza ndani ya ndoa, Didasi akaanza
.


kujisahau baadhi ya majukumu yake ya muhimu. Uwanjani akawa hachezi vile inavyotakiwa kama mwanzoni. Ule upendo aliokuwa akiuonyesha alipunguza, usiriazi ulianza kutawala ndani ya nyumba. Kila nilipomuuliza, ukali ndio ilikuwa silaha yake, kusema kweli sikuwa na kazi na nilibweteka kwavile yeye hakutaka nijishughulishe na kazi. “Humu ndani hakuna chakula? Huvai vizuri? Sikupatii pesa za matumizi?” hayo ndio yalikuwa maneno yake kila nilipohitaji tukae chini tuyazungumze na ikiwezekana kama ni tofauti tuzimalize.

Usiku ambao sitousahau, ni ule alioamua kulala kabisa nje ya ndoa bila taarifa yeyote. Wala haikuhitaji elimu wa upelelezi ili kutafsiri kilichoendelea, jogoo wake alikuwa ameshatumika na mwanamke mwingine. Iliniuma kwasababu kwenye akili yangu nilishajiwekea kwamba moyoni mwake mimi pekee ndio mzuri, na hawezi kunisaliti. Kwavile nilimpenda, sikukubali nishindwe kumrekebisha, yalinijia mawazo mengi sana ila sikutaka kukurupuka.

Hali ya kutolala nyumbani ilizidi, shoo nikawa napigwa ya kawaida tu, yaani ni kama nilikuwa namalizia makombo. Kuna siku nyingine nilikuwa sitosheki na jogoo, kumwambia ndio hivyo niliogopa. Simu yake ilianza kuwekwa ‘pasiwedi’ kila mahali, nilijua tu matumizi sahihi ya jogoo, yamepelekwa kwa mwanamke mwingine. Nikaanza kuwa mtu wa kulia tu maana nilimpenda sana Didasi.

“Hivi unafikiri shemeji yako katulia, unadhani ni bure?”
“Ulimfanyaje Jamani?”
“Kwanza lazima nijue vitu Fulani hivi shosti yangu, maana sisi wanawake wazuri tuna matatizo yetu,”
“Vitu gani sasa!”
“Kweli unampa yote? Kiuno kinafanya kazi kweli hiko? Unamnyonya jogoo wake au ndio unamkaribisha tu aingie wanguwangu?”…
.
.

“Vyote hivyo nafanya shosti yangu, sijui mbuzi kagoma kwenda, nguruwe kakata kamba, kuku kataga juu ya mti, kobe juu ya reli, yaani kila mtindo anaufaidi,”
“Basi sikiliza nikwambie,”
“Nakusikiliza,”
“Wanaume wote baba yao mmoja, mwanaume mwenye akili hata kama amechepuka, lazima amheshimu mkewe ndani ya nyumba na kulinda asijulikane, kuchepuka kwa mwanaume ni lazima, tena usijihangaishe kushindana naye kabisa!”
“Ina maana huyu wa kwangu ni mjinga sio? Maana hata heshima ndani hana tena, kweli kwa uzuri wote huu mi ni kutafutiwa mwanamke mwingine?”
“Wanaume ndivyo walivyo! Sasa nakufundisha uchawi shosti,”
“Uchawi tena?”
“Ndio, ila mpaka tuonane.” Huyo alikuwa ni Martha, rafiki yangu kipenzi, sikumpinga, tulipanga kuonana ana kwa ana ili anieleweshe vizuri kwanini shemeji yangu ametulia kwake.

Lakini kabla ya kuonana na Martha, siku hiyo niliamua kujaribu kitu kwa mume wangu. Nilijishusha na kuwa mdogo kama pilitoni ili nililolitaka lifanikiwe. Niliandaa uwanja wa mapambano ya kikubwa vizuri kwa kuutandika shuka jeupe lenye maua mekundu, nilimpikia chakula kizuri akipendacho, wali wa njegere na nyama ya kuku iliyoungwa na nazi. Nilijibebisha siku hiyo huku nikilazimisha tabasamu usoni mwangu.

Muda wa mechi ulipofika, kwa mitego yangu tu ya ndani ya mtandio nikijifanya kama nataka kwenda kuoga, yeye mwenyewe jogoo aliwika na kuanza kukukuruka ndani ya bukta yake aliyoivaa. Tayari nilishamvuta mpaka uwanjani,
“Kwahiyo unaenda kuoga?” aliniuliza baada ya kuona sieleweki, mara nikae kitandani, mara ninyanyuke na kwenda kujiangalia kwenye kioo, na nilifanya hivyo makusudi mpaka kuokota vitu nilivyovidondosha makusudi ili ashuhudie uzuri wangu, jinsi nilicyobarikiwa chura laini yenye kunesa hata kama nikicheka tu maana nilihisi pengine ameshasahau uzuri wangu.
“Najiuliza hapa sijui niende! Naona uvivu,” nilimjibu kwa sauti ya kimahaba
“Nenda ukaoge bwana,” alinijibu jibu ambalo sikulitegemea
“Ngoja nijilaze kidogo.”
Muda huo naye alikuwa hapo kitandani, nikajilaza kifudifudi, yalikuwa ni makusudi tu, lengo langu nimtege na chura yangu, kwa mwanaume yeyote rijali, asingeweza kuvumilia kukaushia tunda tamu lililoiva tayari kwa kuliwa.
.
.

MWISHO




Blog