MTUNZI : GEOFREY MALWA
“Kurithiwa!”
“Ndiyo,”
“Hizo mila hapana,”
“Kwetu wamezishikilia mno,”
“Sasa kwa usomi huo unashindwa kufanya jambo?”
“Lipo na ndio maana nataka unisikilize,”
“Enhe…”
“Kwetu mtoto wa kiume ni mimi peke yangu,”
“Hiyo inamaanisha kwamba hakuna wa kunirithi siyo?”
“Ndiyo, Kwahiyo ukiulizwa na wazazi wangu wewe kubali kuwa nikifa utarithiwa kwasababu hakuna wa kukurithi,”
“Hapo sawa,”
“Kuna mtoto wa mama mkubwa alitumia hiyo mbinu na ikafanya kazi,”
“Kwani alikufa?”
“Ndiyo, na mkewe mpaka sasa ameolewa na mwanaume mwingine aliyempenda.”
Maongezi hayo yalikuwa kati ya Yuyu na Farkao, mke na mume watarajiwa. Farkao kabla hajampeleka Yuyu nyumbani kumtambulisha, alimuweka wazi juu ya mila zao.
Yuyu alipopelekwa kutambulishwa alikubali kwa moyo mweupe kuwa ikitokea mumewe akafariki basi atakuwa tayari kurithiwa. Basi taratibu za ndoa zilifuata, mahari ikalipwa, ndoa ikafungwa. Ilikuwa ndoa ya maana kweli. Ilifungwa kijijini kwa kina Farkao.
Maisha yalianza ndani ya ndoa, Farkao na Yuyu walikuwa wakiishi mjini, hawakuwa na pesa nyingi bali waliishi kwenye nyumba nzuri waliyopanga na pesa ya kula na kuvaa haikuwapiga chenga kwani Farkao alikuwa akifanya kazi ya udaktari.
Siku moja Yuyu akiwa amekwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani, alikuwa na gari binafsi. Vijana baadhi walimsaidia mizigo kuibeba mpaka gari lilipo. Alipowashukuru hao vijana, ile anataka kufungua mlango kuna mu alimpita nyuma yake kisha akawahi kumfungulia mlango huo wa gari,
“Karibu,”
“Wewe ni nani?”
“Mimi ni mgeni ambaye iko siku Mungu akipenda nitakuwa mgeni wako na utanifungulia mlango wa chumbani kwako kama nilivyokufungulia mlango wa gari…” aliposema hivyo aliondoka, alikuwa ni jamaa fulani mbavu, mwili ulishiba kimazoezi
“Pumbavu kweli, amechanganyikiwa nini!” Yuyu alishangaa hivyo huku akimwangalia huyo jamaa alivyokuwa akiishia.
Yuyu alikuwa ni mrembo, kitu kikubwa alichobarikiwa ambacho ndicho kilimfanya Farkao kumuweka ndani ni tabia, alikuwa ni mtu wa kujali na mpole hasa kwa mumewe. Alipenda sana amani, hii ilimfanya kuwa mtu namba moja ndani ya nyumba kuhakikisha kuna amani hata kama kosa sio lake.
Miezi ilipita, sita ndiyo ilikuwa idadi yake. Nusu mwaka...
na bado hakukuwa na dalili zozote za ujauzito, kelele zikaanza kwa ndugu, mawifi na mama mkwe dhidi ya Yuyu. Walimuandama mno, nafuu kwa Yuyu ni kwamba kelele hizo zilikuwa kupitia simu maana kila mtu aliishi kwake.
Walishindwa kuelewa kuwa mtoto ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu na hutoa muda ambao kwake huona ni sahihi.
Miezi kumi na moja ilipotimia, Farkao akaanza kuumwa. Aliumwa mno, akalazwa hospitarini, kila walipompima halikujulikana tatizo, alikonda mno, ndugu zake ikabidi waje mjini kwa ajili ya kuungana na Yuyu kumuuguza, alikuja mama mkwe pamoja na wifi wa Yuyu.
Wakati wakiwa hapo hospitari, alikuwa jamaa mmoja kumuona mgonjwa, aliwasalimia kwa heshima, Yuyu alipomuona alimkumbuka, ndiye Yule ambaye miezi kadhaa iliyopita wakati akiwa anataka kufungua mlango wa gari kule sokoni alimfungulia na kumweleza kuwa iko siku atamfungulia mlango wa chumbani.
Aliwashangaza wote maana hawakumjua. Alisema kuwa yeye ni rafiki wa Farkao na amekuja kumjulia hali. Alipotoka na Yuyu naye akamfuata kwa nyuma,
“Wewe! Mbona sikujui?”
“Hujawahi kuniona?”
“Nawajua marafiki zake Farkao wote, wewe ni nani?”
“Mimi ni shemeji yako, ni mdogo wake Farkao, sijawaambia ukweli pale kwani nawaona mko katika matatizo mazito,”
“Farkao hana mdogo wa kiume,”
“Ni kweli, hata wao walijua hivyo, anayeujua ukweli ni baba peke yake,”
“Mh! unasema kweli?”
“Ndiyo, nisamehe nilivyokwambia vile maana nilizijua mila potofu za kijijini kwetu,”
“Sawa.”
Basi Mungu naye si athumani, akampenda zaidi Farkao, mwisho wa Farkao ukafikia. Yuyu alilia sana, kuzimia kwake ikawa ni kawaida kwa zile siku za mwanzo, hata mazishi hakuyashuhudia kwani alikuwa amepoteza fahamu.
MWAKA MMOJA BAADAYE.
“Mrithi yupo, kwanini anyimwe haki yake ya msingi?”
“Mama, mimi siwezi kurithiwa,”
“Unasemaje wewe? Usitake nikamkumbuka mwanangu, siku ile ulivyokubali ulikuwa unatuchezea akili?”
“Binti, lazima urithiwe, Ungekuwa hutaki usingekubali na tusingekutambua kama ni mkwe wetu,”
“Lakini…”
“Hakuna cha lakini, taka usitake lazima utarithiwa tu…”
Yuyu baada ya kukazaniwa hivyo aliondoka sebuleni na kukimbilia chumbani,
“Mfuate mwenzako na wewe…”
Kinachu aliambiwa hivyo na baba yake,
huyo kinachu ndiye Yule jamaa aliyekutana na Yuyu kule sokoni, alithibitika kweli ni mtoto wa familia hiyo hivyo kuwa na haki ya kurithi mke wa kaka yake katika hali kama hiyo
Kinachu alisita mwanzoni lakini kupitia msisitizo wa baba yake alikubali. Moja kwa moja mpaka chumbani kwa Yuyu bila hodi,
“Si ungepiga hodi jamani!”
“Samahani, malizia kuvaa…”
“Toka nje sasa,”
“Nimegeukia pembeni, nataka tuzungumze mambo…”
Kinachu alipoingia alimshuhudia Yuyu akiwa ndani ya nguo ya ndani pekee, alizishuhudia zile chuchu za Yuyu, umbo la mwanadada huyo jinsi lilivyojaa ujazo tamanishi, kile kitovu chake kilivyoingia ndani kilimpa hamasa Kinachu, mtoto alikamilika kila idara, kwa haraka Yuyu alivalia tu khanga moja akijua atamsikiliza Kinacho kwa muda mfupi,
“Haya sema!”
“Naomba uje ukae hapa kwenye kochi tafadhari,”
“Hapana, nitaketi hapa kitandani, wewe keti kwenye kochi,”
Basi Kinachu aliketi kwenye sofa zuri kubwa lililokuwa hapo chumbani huku Yuyu sasa…mtoto aliketi kitandani, hipsi alikuwa nazo, wowowo lilikuwepo la wastani, ile khanga hata haikumtosha vyema, aliilazimisha ifunike mapaja yake mazuri yaliyonona lakini haikutosha, Kinachu aliendelea kufanya utalii wa bure huku mdudu wake ukiitika bila kuitwa kwenye suruali yake.
“Sawa, una mpango upi juu ya walichoongea wakwe zako?”
“Kwakweli nimechanganyikiwa, hata sielewi,”
“Kuchanganyikiwa sio mpango,”
“Nilikubali kwavile nilijua hakukuwa na mrithi, siwezi kurithiwa,”
“Hata mimi siwezi kurithi, naona huna mpango ngoja nikupe,”
“Enhe…”
“Niliwasikia wakiongea kuwa baada ya mwezi wanaondoka wanaelekea kijijini, Kwahiyo tuwaigizie kwa huu muda mfupi,”
“Kwani tusipowaigizia nini kitatokea?”
“Hutatamani kujua,”
“Kwanini?”
“Nadhani umeshawahi kufika nyumbani kule kijijini,”
“Ndiyo,”
“Uliwaona wale wakinamama wawili waliokuwa kama wana akili za kitoto?”
“Ndiyo, walikuwa wakiishi nyumba ya jirani,”
“Basi wale walipatwa na hiyo hali baada ya kukataa kurithiwa, pale ulipokubali kuwa uko tayari kurithiwa uliweka agano na mila zao, ukienda kinyume lazima litakukuta jambo, ila ukifanya kama ninavyosema, utawaepuka,”
“Mh! sasa hayo maisha ya maigizo ndio inakuwaje?”
“Ni magumu lakini ndio njia pekee, tutalala chumba kimoja,
MWISHO