MTUNZI : GEOFREY MALWA
Maisha! Maisha! Maisha! Nimekuita mara tatu. Maisha ndio maana hufananishwa na sahani pana yenye kila kitu. Leo niko tayari kuwasimulia mkasa huu ambao nimeupa jina la DOGII, nikisema hivyo najua mmenielewa jamani, maelezo zaidi yapo ndani ya mkasa huu kuhusu hilo neno Dogii.
Naitwa Mehmetina, kifupi waliniita Meti, nililipenda sana hilo jina, dada yangu kipenzi ambaye ndiye chanzo cha mkasa huu aliitwa Lanovabi, yeye kifupi walimuita Vabi. Nilimpenda sana dada yangu mpaka kufikia hatua ya kulipiza kisasi kwa ajili yake juu ya mtu aliyempenda sana miaka mitatu iliyopita.
MERERANI
Ndipo nilipokwenda kutafuta maisha, nilifikia kwa rafiki yangu ambaye naye alikuwa na malengo kama yangu, aliitwa Snea. Kwanza hiyo siku nafika, sikuja kupokelewa bali nilielekezwa tu nikapanda bodaboda, hapakuwa ni sehemu inayochanganya mpaka inifanye nipotee.
"Nikaeje bwana wakati nimekwambia nina mgeni!"
"Dogii,"
"Unamwaga saa ngapi?"
"Sasahivi bwana, ukinipa yale mauno yako hata dakika simalizi,"
"Sawa, uaichelewe babaa."
Niliyasikia hayo maongezi ambayo wala sikuhitaji mkalimani ili anitafsirie yaliyokuwa yakiendelea. Nilisikia kelele za mchi ukitwanga, na baada ya muda sifa juu ya kiuno cha rafiki yangu nilizisikia, dakika mbili zilikuwa nyingi, kidume aliunguruma na mwishowe nikasikia mlio wa kofi, bila shaka shosti alipigwa kwenye mnofu wa kalio.
"Ahsante bebi, nakupenda sana,"
"Nakupenda pia."
Hayo yote nilisikia, na begi langu dogo la mgongoni niliendelea kusubiri hapo nje,
"Meti dia! Pole jamani nisubiri kidogo mamii," aliniambia hivyo Snea nami nikamwitikia vizuri ili aone nimeona kawaida tu hiyo hali.
Bila shaka waliekea kuoga, baada ya muda jamaa akatoka, akanisalimia, jinsi alivyoniangalia tu nilijua hajatulia. Baadaye Snea pia alitoka na kunikaribisha ndani.
"Mamaa wa Dogii," nilimtania
"Shoga yangu huna dogo!"
Tulicheka kwa pamoja ambapo kusema kweli mambo yalikuwa ni mengi sana ya kuongea. Nilikaribishwa bafuni ambapo wafukunyuanaji walitoka huko muda usio mrefu.
Nikiwa nabadili nguo baada ya kutoka bafuni, nilisikia sauti ya kiume sebuleni ambayo ni kama nilikuwa naijua hivi,
"Jana kuna chalii ameotea jiwe naye akaotewa,"
"Jamani,"
"Yaani huku usipokuwa mjanja hutoboi, utakuwa unawafanyia kazi watu wengine tu,"
"Sema alikuwa bado mtoto wa mama,"
"Ndio hivyo."
Niliwasikia wakiongea hivyo ambapo nilipotezea na kuendelea kuvaa. Kwavile tayari yalishafika majira ya jioni, nilivalia traki kujikinga na baridi, nilipofika sebuleni, ndipo nilihakikisha,
"Eh! Mwenyezi Mungu anipe nini jamani?" Alisema huyo kaka,
Nilimfahamu kwa jina la Panzi, sikuwa hata na masaa sita tangu nimelifahamu jina lake, nilikutana naye niliposhuka tu kutoka kwenye gari pale stendi, alikuwa jasiri, alinifuata na kuniambia,
"Karibu mererani, wewe ni msichana mrembo sana, unaitwa nani?"
"Kwini," nilimdanganya jina
"Jina limefanana na wewe kabisa, umenivutia ila sitakwambia nakupenda, tukionana kwa mara ya pili popote pale, nitajua kuwa wewe ni halali yangu," nilitabasamu kisha nikamjibu
"Nakutakia bahati njema,"
"Sawa, nakuahidi nikikutana na wewe kwa mara ya pili nitakukiss kabisa,"
"Sawa, nakutakia bahati njema."
Tulivyoongea hivyo aliondoka na kupanda basi, nilicheka maana nilijua ni wapi atanionea tena,
"Kwani mnafahamiana?" Snea alituuliza
"Simfahamu," nilijibu
"Jamani, kwani humu ndani kuna dada yake Yuda? Mbona nakanwa mbele ya umati,"
"Panzi acha kujichetua, ndio kwanza huyu mrembo amefika leo,"
"Nilichokiahidi lazima nikitimize."
Aliposema hivyo Panzi si akainuka bwana! Nikajua masihara, alinifuata kisha akanipa mkono, nilipoushika alinivuta na kunibusu shingoni,
"Nilijua tu wewe ni wangu," Panzi alisema hivyo
Nilimsukuma na kujitoa kwake, nilimkaripia kwa tabia hiyo na kumtaka asirudie tena, Snea pia alimkaripia, basi Panzi aliomba msamaha na nikamsamehe. Alipoondoka ndio nikaanza kumhadithia Snea ilivyokuwa, tulibaki tukicheka sana.
Nikawa nasoma ramani ya namna ninavyoweza kupata pesa maana sikutaka kutegemea pesa kutoka kwa mwanaume. Nilitaka kuzitafuta pesa za kwangu tu kwa jasho langu.
Snea ndio alikuwa mwalimu wangu, kabla sijaja alikuwa akiniambia kuwa alikuwa akiingia machimboni yeye mwenyewe lakini nilipokuja sikushuhudia hivyo, yeye alimlenga mwanaume mjanja mwenye kujituma kwahiyo wakawa wanatunza wote madini wanayoyapata.
.
.
Pia akanishauri nifanye hivyo, yaani nitafute mwanaume wa aina kama yake, baada ya muda nitaondoka Mererani nikiwa na utajiri mfukoni, tena hakushia hapo alimpendekeza Panzi kama ndiye sahihi kwangu.
Ni kweli Panzi alikuwa sio haba, yaani ni aina ya wanaume ambao wanajua kujali wanawake. Alikuwa akiniletea zawadi mara kwa mara, hakuchoka kunitongoza, udhaifu wangu wa upweke ukaanza kunigharimu, muda mwngi yeye ndio alipatikana kuliko Snea aliyekuwa ana harakati nyingi kupita maelezo.
Mwezi ulipita bila Panzi kukoma kunifuatilia, hakuwa Panzi peke yake lakini yeye ndiye aliyekuwa anapata nafasi nzuri ya kuongea na mimi kuliko mwingine kwasababu alikuwa akijuana na Snea.
Siku moja nikiwa nimeboreka maana sikuwa na marafiki zaidi ya Snea. Wawili wapendanao walikuwa ndani wakipeana mapenzi muda huo, kila kitu nilikisikia, ni muda mrefu sijakutana na mwanaume,
"Ooh ssss bebi una obo tamu, aammm hivyo hivyo taratibu, zungusha kiuno, aaah(Tusi la nguoni) unanifaki vizuri jamani, sikuachii..." Yaani Snea hakuacha kuongea kabisa, huyo mwanaume wake ndio kama cherehani yaani alielezea kila kitu...
Nikiwa nimetulia hapo kochini, nilivalia sketi fupi na sweta kaba shingo lililonikaa vyema. Panzi akanipgia simu, nilipopokea alinishtua,
"Samahani Kwini naomba uje au uniagizie bodaboda naumwa sana,"
"Uko wapi?"
"Nyumbani, ukiwa umebanwa na shughuli basi mtafute bodaboda anipeleke hoapitari." alikata simu baada ya kusema hivyo, sauti yake ya kutetemeka ilnishtua, nikataka niashtue wapendanao lakini ikanibidi nichukue hatua, nikatafuta bodaboda haraka ikanipeleka mpaka nyumbani kwao,
"Twende wote," nilimwambia hivyo bodaboda
"Kwanini? Amezidiwa sana?"
"Ndio." Nilimdanganya, niliogopa kuingia peke yangu maana tabia ya wanaume naijua, anaweza akasingizia ugonjwa kumbe ni mtego akuhondomole.
Nyumbani kwake hapakuwa mbali sana, yeye alipanga nyumba yenye vyumba viwili, sebuleni, jiko, choo na bafu ilikuwa ndani. Ni siku moja tu nilienda nyumbani kwake nikiwa na Snea, ndio maana nilipajua.
Ile nafungua tu mlango ilibaki kidogo nikimbie, nilishtuka na kubaki nimeshika mlango kama mtu aliyetaka kudondoka chini na kutumia mlango kama kiegamo.
.
MWISHO