MTUNZI : GEOFREY MALWA
Binadamu kabla hujafa hujaumbika. Walisema hivyo wahenga kutokana na uzoefu wa maisha waliyopitia. Mtu ukifanikiwa katika maisha ni wazi kuwa unakuwa na malengo yako uliyojiwekea, lakini amini nakuambia kama lengo la kuisaidia famili yako halitakuwepo basi utakuwa unafanya kazi bure.
Mungu hutubariki ili tuwasaidie wengine, kwa kukwepa kufanya hivyo lazima adhabu itatukuta. Kuwa nami katika simulizi hii itakayokusisimua na kukufurahisha sana pia kukuachia funzo kubwa katika maisha yako.
“Mungu amekujaalia pesa lakini busara umekosa,”
“Mdogo wangu, makosa nilishafanya, hata ukinilaumu hatuwezi kumrudisha marehemu,”
“Unaona! Eti unaita marehemu! Sema marehemu mama, aliyekufa ni mama yako mzazi Donadi, ni mama yako,” alianza kulia baada ya kusema hivyo
“Jamani, inabidi tufikie muafaka hili suala, ninyi ni ndugu hamuwezi kuwa hivi milele,”
“Hata kama, aniache na maisha yangu ya hapa kijijini, yeye akafurahie maisha yake ya hela huko mjini, hayo si ndio yanayompa kiburi,”
“Mdogo naomba unisamehe, usije ukafikiri sikumtambua kama mama, nakuomba sana Kolebe,”
“Mjini siendi, nimebariki nendeni tu.”
Mzozo huo ulikuwa kati ya Ndugu Wawili, Donadi na Kolebe waliozaliwa na mama mmoja ila mmoja alikaa sana na mama kijijini mwingine alikulia mjini kwa baba yake. Huko alikuwa na maisha mazuri, tofauti yao ni kwamba kila mmoja alikuwa na baba yake.
Kolebe alikuwa akimlaumu kaka yake kuwa pamoja na kuwa na pesa nyingi ila alithubutu kumwacha mama yake mzazi afe kwa kukosa matibabu. Ni jambo ambalo lilimuuma sana Kolebe.
Wazee waliingilia kati hapo kijijini na kufanikisha kurudisha amani baina ya wawili hao. Wakapatana baada ya kama kupita wiki hivi. Akachinjwa mbuzi na wote wakashiriki pamoja na wazee wa kijiji.
“Sasa mdogo wangu, sitaki kurudia makosa, nataka twende wote mjini, kule utapata kazi ya kufanya na utakuwa na maisha mazuri,”
“Sawa, litakuwa ni jambo jema.”
Basi Kolebe pamoja na kaka yake ambaye aliambatana na mkewe aliyeitwa Lashki, walirejea mjini na maisha yakaanza.
Kolebe alishazoea kuamka asubuhi na kufanya kazi, hivyo hakuacha hiyo tabia, alifanya hivyo hata alipofika mjini, asubuhi walipoamka walishangaa,
Kolebe alishafanya shughuli nyingi sana. Zipo alizokuwa amefanya sahihi na zingine alikosea kutokana na ugeni wa nyumba ya kifahari.
Walimcheka lakini walimwelekeza na kumzuia siku nyingine asifanye shughuli nyingi hivyo. Kama kawaida Donadi kila siku lazima ahudhurie kazini kutafuta mkate wa kila siku.
Kolebe alikuwa ana vituko sana, Lashki alikuwa akicheka tu, kuna muda alimpigia mumewe ‘video call’ basi Kolebe alikuwa akishangaa tu na kufurahia.
Lashki aligundua jambo, Kolebe alikuwa na ugwadu uliopindukia, sasa kwa mjini Lashki alikuwa akijiachia kimavazi japo sio sana. Kama siku hiyo ya kwanza alivalia gauni lililokuwa fupi lakini aliongeza kujisitiri na khanga. Kwa jinsi alivyobarikiwa mwanamke Yule, ni kama hakujisitiri, Yaani hilo wowowo ni meng’enyu meng’enyu.
Muda mwingi akimsogelea kama ule muda aliokuwa akiongea na Donadi kwa ‘video call’ alishuhudia kabisa vuvuzela la kolebe likiwa limetuna na lilimshtua kwasababu lilikuwa limeshiba haswa.
Ilipofika jioni majira ya saa kumi na moja, kila mmoja alikwenda chumbani kwake kujipumzisha, kila mmoja alimuwaza mwenzake katika kona tofauti, Kolebe alitawaliwa na mawazo ya jinsi shemeji yake alivyo mzuri, mweupe, mrefu, wowowo, jinsi kiuno chake kilivyotumbukia ndani na kupisha wowowo kuchukua nafasi yake. Ile sauti yake akiongea, akicheka na mwili unavyomumukwamumukwa.
Huku kwa upande wa Lashki kidogo ilikuwa ni tofauti. Yeye alikuwa ameinamia simu janja yake akiwa anatumiana jumbe na rafiki yake wa sirini na uwazini. Walibebeana siri nyingi sana marafiki hao na walidumu kwa muda mrefu bila migogoro makubwa.
“Kwahiyo shemeji ana ukame!”
“Hatari, yaani huyu nikileta mazoea naye anaweza akanibaka,”
“Na kweli, huwa zinawakamata vibaya!”
“Unashangaa kwenye kona umebananishwa mwenzangu!”
“Uvimbe anao lakini?”
“Kha! Kamzidi hadi kaka yake, dume lina vuvuzela lililoshiba hatari,”
“Bwana we! Ukae makini,”
“Mimi sina shida hata iweje siwezi kufikia kumsaliti Donadi, nimetoka naye mbali sana,”
“Kwanza sio maadili, ndugu kuwachanganya!”
“Kabisa, baadaye nitakuja kudharirika mimi,”
“Kabisa shoga yangu, sema huyo inabidi umlengeshee demu apunguze ugwadu,”
“Mh! Demu gani mwenzangu, wasichana wenyewe
.
hawa wa sasahivi, kwanza magonjwa, labda atafute yeye mwenyewe,”
“Hilo neno nalo.”
Baada ya soga hizo kilichofuata kilikuwa ni umbea mwingine usiohusu Kolebe tena.
Tukirudi huku kwa Kolebe, alipigiwa simu na binamu yake, simu yenyewe jamani, Yaani kama ni mtu ungesema ni majeruhi anakaribia kufa kwa bendeji alizofungwa, simu ni kama iliokotwa, ilizungushiwa gundi ya karatasi, kwanza kuipokea alichukua peni na kubonyeza maana haikuwa na batani,
“Binamu!”
“Nani binamu yako!”
“Umechukia kwanini?”
“Kwahiyo ndio umetuacha na maisha yetu ya shida ukaenda mjini,”
“Kaka alitaka iwe hivi,”
“Hakuna, sio kaka yako, kwanini usingekataa?”
“Sikuwa na namna,”
“Hivi ndivyo ulivyoniahidi?”
“Najua, ngoja nitafute kisha nitarejea,”
“Wewe sikia, usijisumbue, sikutaki tena na huyo kaka yako atasimulia,”
“Binamu, binamu! Gwamaluko! Hello Gwama!”
Tayari Binamu gwamaluko alishakata simu, alichukia sana, Kolebe alimuahidi kuwa atamuoa, walizoea kuishi maisha ya shida pamoja, kitendo cha Donadi kumchukua Kolebe alikitafsiri kama usaliti.
BAADA YA WIKI
Mdomoni mwa shemeji ni jina la Donadi ndilo lilikaa, hakutaka kumsikia mtu yeyote yule. Akili yake ni kama ilichanganyikiwa, Kolebe ndiye aliyekuwa na uwezo wa kumlisha, Yaani Kolebe ndio alimuita Donadi Halafu Donadi akawa Kolebe.
Lilikuwa ni jambo lililowashangaza wengi sana, ni kipi kilimpata Lashki, akili yake haikuwa sawa, aliweza kufanya vit vingi lakini Kolebe akiwepo, akikosekana ni ugomvi mkubwa. Hilo jambo mwanzoni Donadi alilichukulia kawaida lakini kadri siku zilivyokwenda lilimchukiza sana maana alihisi anakwenda kupoteza nafasi ya mume.
Walirejea nyumbani wakitokea hospitarini huku Lashki akiwa pembeni ya Kolebe. Wakati matatizo hayo yanamkumba Lashki, kazini ikatokea safari ambayo hakuweza kuipangua, ilimlazimu Donadi kusafiri richa ya kuwa katika kipindi kigumu,
“Sikia mdogo wangu, hakikisha shemeji yako unamheshimu,”
“Sawa kaka usiwe na shida,”
“Narudia tena, shemeji yako mheshimu, nitakuwa nikipiga simu hii mara kwa mara, uwe unapokea nawaona sawa?”
“Sawa.”
Donadi alimfundisha Kolebe namna ya kupokea simu ‘WhatsApp video call’ mpaka akaweza, halikuwa jambo jepesi hata kidogo kwa Donadi kumuacha mkewe
.
MWISHO