Search This Blog

Saturday, July 23, 2022

2

 NBC YAIMWAGIA TAYOA MSAADA WA SHS MILIONI 100 November 27, 2013, 5:20 am Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga Melu kusaidia mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA). Hafla ilifanyika wakati wa tukio la uzinduzi wa mradi huo unaodhaminiwa na NBC jijini Dar es Salaam jana. Katikani ni Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi. Mizinga Melu (katikati) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi wa tofuti ya vijanatz.com ikiwa na habari kuhusu ajira (kazitz.com), fedha (fedhatz.com) na ujasiriamali (biasharatz.com). Hafla hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana  wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA) unaodhaminiwa na NBC. 3: Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu akishikana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika baada ya kukabidhi  mfano wa hundi ya shs milioni 100 zilitotolewa na benki hiyo kusaidia mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA). Hafla ilifanyika wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaodhaminiwa na NBC. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo aya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula Mfugale. Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa TAYOA, Peter Masika (kushoto), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa NBC, William Kallaghe wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu akizungumza na vijana na wageni wengine kuhusu huduma za kibenki na kuhusu mikakati ya benki kusaidia suala la ajira na ujasiriamali kwa vijana katika hafla hiyo. Wasanii wakitoa burudani kusindikiza uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya masuala ya ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Shirika la kuelimisha vijana nchini (TAYOA) unaodhaminiwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam Previous Article Next Article WASHINDI WA DROO NDOGO YA CHAMPIONI 'SHINDA MAHELA' WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO November 27, 2013, 5:23 am Clement Michael (kulia) ambaye ni mkazi wa Mbagala-Zakhem, Dar, akikabidhiwa Sofa Set yake na Mr Championi. Clement akichekelea baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Sofa Set leo nje ya ofisi za Global Publishers zilizopo Mwenge, Bamaga jijini Dar. Bashir Hassan (kushoto) mshindi wa friji akikabidhiwa zawadi yake na Mr Championi nje ya ofisi za Global Publishers. Radephili Mcharo (kushoto) akikabidhiwa jezi yake na Mr Championi. WASHINDI wa Droo Ndogo ya Promosheni ya Shinda Mahela na Championi, leo wamekabidhiwa zawadi zao nje ya ofisi za kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa washindi waliofika kuchukua zawadi zao ni Clement Michael mshindi wa Sofa Set, Bashir Hassan aliyejishindia Friji na Radephili Mcharo aliyejinyakulia Jezi. (PICHA NA ISSA MNALLY / GPL) Previous Article Next Article KINANA AIJIA JUU SERIKALI,AITAKA IACHE URASIMU NA UMANGIMEZA KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO YA WANANCHI November 27, 2013, 5:34 am Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga moja ya nyumba ya waalimu katika shule ya sekondari ya Ikuti iliopo katika kata ya Ikuti,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya mapema leo,akiwa sambamba na Ujumbe wake hawapo pichan,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Asharose Migiro.Kinana na Ujumbe wake wako ziarani Wilayani Rungwe Magharibi mkoani Mbeya,ambapo kesho watakuwa wilaya ya Ileje kutekeleza Ilani ya chama,kukagua miradi ya chama na wanachi sambamba na kujua na kutatua matatizo yao kwa namna moja ama nyingine. Wakienda kukagua moja ya bweni la kulala wanafunzi wa shule hiyo ya Ikuti. Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa ,Asharose Migiro wakielekea kuonana na balozi balozi wa shina la Kitonga,ndani ya kijiji cha Ikuti,Bwa.James Mbasi ,pichani nyuma anaefuatia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnaupe Katibu Mkuu wa CCM,pili kushoto,Ndugu Abdulrahman Kinana na wajumbe wake  wakielekea kuonana na balozi wa shina la Kitonga,ndani ya kijiji cha Ikuti,Wilayani Rungwe mapema leo. Pichani ni Katibu Mkuu wa CCM pichani kati,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kilichopo kwenye zahati ya Ikuti,katika kijiji cha Ikuti wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Kada maarufu wa CCM,Richard Kasesela akipiga ngoma ya asili ya kinyakyusa iitwayo Lipenenga. Baadhi ya vijana mbalimbali wakiwa juu ya miti wakifuatilia mkutano wa hadhara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia jioni ya leo kwenye kijiji cha Ikuti. Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Asharose Migiro akizungumzaa mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnaupeakizungumzaa mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Wilayani Rungwe. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,kwenye mkutano wake wa hadhara . Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akifafanua jambo kwa wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Mbunge huyo pia aliwataka akina mama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali,ili kurahisishiwa kupata mikopo ya kuendeleza miradi yao ambayo wataianzisha katika suala zima la kujikwamua na ugumu wa maisha, Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Iponjora,Wilayani Rungwe,Kinana aliwaasa wafanyabiashara hao kutokuwa na tamaa ya kuuza biashara yao hiyo ya ndizi kwa bei ya kutupa,badala yake waachane na watu wa kati,wafanye biashara yao kwa faida na si kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa,ambao hawajui ugumu wa kilimo cha zao hilo,Kinana katika kuwaongezea kasi ya biashara yao ya ndizi aliwachangia kiasi cha shilingi laki moja Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro akizungumza na wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Iponjora,Wilayani Rungwe,mkoani Mbeya. Wakazi wa kijiji cha Ikuti wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe mara baada ya kuusimamisha msafara wake. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema leo,Kinana alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kutatua tatizo sugu la Maji na Barabara katika kijiji hicho,alichozaliwa Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa.Aidha kinana aliitahadharisha Serikali katika suala zima la kuitaka Serikali iache urasimu na umangimeza katika mipango ya maendeleo kwa Wananchi,kwa sababu Urasimu na umangimeza huo huwanufaisha zaidi wanaoshikilia fedha za miradi hiyo wakati wananchi Wanaumia na kuteseka kwa kukosa huduma muhimu mbalimbali. Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema leo kuhusiana na kero mbalimbali zinazowatatiza wakazi hao,ikiwemo suala la maji na barabara sambamba na tatizo la bei ya zao la ndizi kutoka kwa wakalima kwenda kwa wafanyabiashara. Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa akisalimiaa na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Nje,Dkt Asharose Migiro mara baada ya kukutana katika kijiji cha Lupango,Wilayani  Rungwe,ambapo Ndugu Kinana aliwahutubia wakazi wa kijiji hicho. Pichani shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro walipokuwa wakielekea kukagua jengo la bweni la kulala wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ikuti,Wiayani Rungwe mkoani mbeya leo. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakereketwa wa shina la vijana waendesha boda boda katika soko la Kiwira,ambapo Ndugu Kinana aliwachangia kiasi cha fedha shilingi milioni tano kwa ajili ya kujiendeleza na kuwapa uwezo wa kujikopesha wenyewe katika suala zima la kujikwamua na suala zima la umasikini,hasa ikifahamika kuwa tatizo la ajira kwa vijana limekuwa kubwa. Pichani shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa amepozi na mdau. Previous Article Next Article SIRI 5 ZA MAPENZI ZA WOLPER ZAVUJA - SOMA HAPA November 27, 2013, 6:42 pm MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili. Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi. KISA/MKASA Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma. Jacqueline Wolper Massawe ALIANZIA WAPI NA DALLAS? “Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo, ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu. “Nilimsikiliza sana. Jamani yule mwanaume anaongea kwa ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa aliponieleza kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe). “Mwanzoni nilidhani ni tapeli. Nikamkatia simu. Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu, alinitajia namba zao za simu ambazo ni za kweli. “Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza nyodo zangu. “Aliniuliza nataka anifungulie biashara gani. Nikamwambia biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani. nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki fremu moja, nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna tatizo. “Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar) alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia Mbezi Beach. “Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani? Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema ataninunulia Toyota Harrier. “Kweli baada ya siku mbili-tatu nililetewa Toyota Harrier nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego nikaingia kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea hadi Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha teksi, nikaenda na dereva nikalichukua hadharani ili lolote likitokea nipate msaada. “Nilikabidhiwa funguo za lile gari na documents zake, nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake Dallas alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha akanitumia cheni ya dhahabu. “Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni 15 nipeleke nyumbani nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye angeenda kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas ambaye walikiri kumfahamu kwa sababu alishawapigia simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.” AMESHAKUTANA NA DALLAS? “Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha nilikuwa natumiwa kila siku. “Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6. “Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile gari nililia sana. Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu inakuja)! “Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend ambaye tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa. Nilimweleza kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa aliumia. “Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana na yule boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu niliamini nimepata mchumba wa kunioa. ATAKIWA KUBADILI DINI “Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa mchumba wake hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na jina langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana maishani mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika dini yangu ambayo mama ni mzee wa usharika na mwimba kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.” NINI KILIFUATA? “Siku moja nilikuwa Tanga nashuti filamu, nilikuwa nikitoka hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu akaniambia yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo Tanga akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga mzigo. Zilipita saa nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu, Dallas alinipigia simu akaniambia ameniona. “Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota Prado. WOLPER MORO, DALLAS DAR “Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda Morogoro, yeye aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana. Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo vituko vikawa juu ya vituko. “Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa na mwanamke au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho alikuwa katika swaumu hivyo akionana na mimi nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu). BADO HAWAJAKUTANA? “(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na amejaa tele kwenye kumbi za starehe. “Baada ya kumaliza swaumu, siku moja aliniambia anakuja nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi chumbani. Nilitandika mashuka meupe kitandani na kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana nikakaa kama malkia nikimsubiri mchumba. “Huwezi amini, hadi giza linaingia Dallas hakutia mguu. Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona huyo mchumba? Ninyi acheni tu! “Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara alikuwa anafanya HATIMAYE WAKUTANA LAKINI… “Nilikasirika sana, nikasema huyu ni mchumba gani asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu,  asubuhi nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’. Nilishajua sauti yake kupitia simu hivyo nilimkaribisha na nguo zake nikaingiza ndani. Lakini cha kushangaza alikuja na pikipiki! “Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna ndugu zake walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu shavuni kisha jioni akaondoka. “Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha akiwa na wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao niliambiwa eti ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa! “Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi. Dallas simuoni. Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama na nikamwambia akachukue nguo zake. UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA “Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi ndiyo nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye nilipopata mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri kwa sababu kanipita umri na ana busara. Tunapendana sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau tukio hilo katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo wangu. (akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu anajua… VIPI KURUDIA UKRISTO? “Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa najifungia ndani nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia kila siku bora nirudi kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa sasa nasali Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema. MBALI NA DALLAS Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua mmoja mmoja. ALI KIBA Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi. KWA NINI WALIACHANA? “Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.” DIAMOND VIPI? “Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper. VIPI KUHUSU JUX? “Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,” alimalizia Wolper ambaye kwa sasa ana mwanaume asiyependa kumwanika. CREDIT: GPL Previous Article Next Article NORA: RAY, JOHARI WANA LAANA YANGU November 27, 2013, 6:54 pm BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao. Akizungumza na mapaparazi wetu hivi karibuni, Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni. “Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na kidole. “Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza kwenye fani. “Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa, mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui zangu wote wataumbuka mchana kweupe,” alisema Nora. Gazeti hili liliposhindwa kumpata Ray kwa kumpigia simu lilimtumia ujumbe ambapo alijibu kwa kifupi. “Dah, kiukweli kama Nora ndiye kasema hivyo basi mimi sina comment yoyote na madai hayo na kirahisi naomba uandike hivyohivyo,” alijibu Ray. Kwa upande wa  Johari alipotumiwa ujumbe aliendelea ‘kunyuti’. Previous Article Next Article MAN UNITED YAFANYA MAUAJI YA KUTISHA LIGI YA MABINGWA, YAWAPIGA WAJERUMANI 5-0 NYUMBANI KWAO November 27, 2013, 6:56 pm MANCHESTER United imefanya mauaji makubwa ugenini, baada ya kuitandika Bayer Leverkursen mabao 5-0 nchini Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya. Mabao ya United usiku huu yamefungwa na Valencia dakika ya 22, Spahic aliyejifunga dakika ya 30, Evans dakika ya 65, Smalling dakika ya 77 na Nani dakika 88. Wayne Rooney ndiye alikuwa nyota wa mchezo kutoka na kupika mabao manne katika ushindi huo ambao haukutarajiwa. Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra/Buttner dk70, Jones, Giggs, Valencia/Young dk80, Kagawa, Nani na Rooney/Anderson dk80. Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Omer Toprak, Can, Bender/Kohr dk81, Reinartz/Hegeler dk70, Rolfes, Castro, Son Heung-min/Derdiyok dk70 na Kiessling. Maridadi: Manchester United imeiangamiza Bayer Leverkusen nchini Ujerumani usiku huu Brilliant: Wayne Rooney supplied four goals in a wonderful performance Brilliant: Wayne Rooney supplied four goals in a wonderful performance Arriving: Antonio Valencia arrives at the back post to convert a measured Wayne Rooney cross to make it 1-0 Arriving: Antonio Valencia arrives at the back post to convert a measured Wayne Rooney cross to make it 1-0 Glance: Emir Spahic is unfortunate to score an own-goal as David Moyes' United team double their lead Glance: Emir Spahic is unfortunate to score an own-goal as David Moyes' United team double their lead Making sure: Jonny Evans scored the third goal, turning in after a scramble from a corner Making sure: Jonny Evans scored the third goal, turning in after a scramble from a corner This one's his: Chris Smalling scored the fourth, with a simple tap-in at the back post This one's his: Chris Smalling scored the fourth, with a simple tap-in at the back post Late goal: Nani latched on to a perfect Ryan Giggs pass to add a neatly taken fifth with just two minutes remaining Late goal: Nani latched on to a perfect Ryan Giggs pass to add a neatly taken fifth with just two minutes remaining Pats on the back: The United No 10 delivered the perfect ball for Valencia to score Pats on the back: The United No 10 delivered the perfect ball for Valencia to score Disbelief: Leverkusen players are stunned after shipping their second goal from a perfect Rooney free-kick Disbelief: Leverkusen players are stunned after shipping their second goal from a perfect Rooney free-kick Finish: Nani adds a late fifth to add a cherry on top of the United performance Finish: Nani adds a late fifth to add a cherry on top of the United performance Vintage: Ryan Giggs started for David Motes - the United legend turns 40 on Friday Vintage: Ryan Giggs started for David Moyes and added a late assist for Nani - the legend turns 40 on Friday Progress: Manchester United players enjoyed a comfortable evening in Leverkusen Progress: Manchester United players enjoyed a comfortable evening in Leverkusen Dejected: Leverkusen players trudge off after a heavy defeat Dejected: Leverkusen players trudge off after a heavy defeat Face in the crowd: Sir Alex Ferguson watches his former team at the BayArena Face in the crowd: Sir Alex Ferguson watches his former team at the BayArena Positive: David Moyes looks on as his team record an impressive victory Positive: David Moyes looks on as United record an impressive victory Anchor man: Phil Jones started in midfield for the Red Devils Anchor man: Phil Jones started in midfield for the Red Devils Powerless: Simon Rolfes and his Leverkusen team-mates struggled to contain Rooney Powerless: Simon Rolfes and his Leverkusen team-mates struggled to contain Rooney Stand him up: Son Heung-Min attempts to take on United's skipper Patrice Evra Stand him up: Son Heung-Min attempts to take on United's skipper Patrice Evra Give him the brush off: Giulio Donati is kept at bay by the arm of Nani Give him the brush off: Giulio Donati is kept at bay by the arm of Nani Sliding in: Patrice Evra makes the tackle on Giulio Donati Sliding in: Patrice Evra makes the tackle on Giulio Donati Starting berth: Shinki Kagawa was granted a place in the starting line-up for the third match in a row Starting berth: Shinki Kagawa was granted a place in the starting line-up for the third match in a row StayingStaying power: Giggs shrugs off a tackle from Gonzalo Castro power: Giggs turns 40 on Friday Staying power: Giggs shrugs off a tackle from Gonzalo Castro Previous Article Next Article MAN CITY YAPIGA MTU 4 - 2 VIKTORIA PLZEN ULAYA November 27, 2013, 6:58 pm MANCHESTER City imeifumua mabao 4-2 Viktoria Plzen Uwanja wa Etihad usiku huu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabao ya City yamefungwa na Aguero kwa penalti dakika ya 33, Nasri dkika ya 65, Negredo dakika ya 79 na Dzeko dakika ya 90, wakati mabao ya Viktoria Plzen yamefungwa na Horava dakika ya 43 na Tecl dakika ya 69. Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Richards, Demichelis, Lescott, Kolarov, Milner, Garcia, Fernandinho/Toure dk65,  Nasri/Negredo dk75, Aguero/Navas dk46 na Dzeko.. Viktoria Plzen: Kozacik, Rajotoral, Cisovsky, Prochazka, Hubnik, Horvath, Horava, Petrzela/Kovarik dk73, Kolar/Bakos dk86, Duris/Wagner dk89 na Tecl. La kwanza: Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza kwa penalti Strike: Horava's equaliser flew in from 25 yards, an unstoppable shot Joe Hart could do nothing about Strike: Horava's equaliser flew in from 25 yards, an unstoppable shot Joe Hart could do nothing about Turns up: Nasri scores to put City 2-1 up at the Etihad in a topsy-turvy encounter Turns up: Nasri scores to put City 2-1 up at the Etihad in a topsy-turvy encounter Super sub: Alvaro Negredo (second right) celebrates scoring the third goal with Jesus Navas Super sub: Alvaro Negredo (second right) celebrates scoring the third goal with Jesus Navas Arise: Dzeko put his case forward for preferential treatment with a superb header late on Arise: Dzeko put his case forward for preferential treatment with a superb header late on Leveller: Tomas Horava wheels away after equalising for Plzen just before half-time Leveller: Tomas Horava wheels away after equalising for Plzen just before half-time Tucked home: The Argentinian slotted home the penalty after a handball in the area, but Plzen soon equalised Tucked home: The Argentinian slotted home the penalty after a handball in the area, but Plzen soon equalised Stretch: Manchester City's Sergio Aguero (left) and Plzen's Vaclav Prochazka battle for the ball Stretch: Manchester City's Sergio Aguero (left) and Plzen's Vaclav Prochazka battle for the ball It's mine: Defender Joleon Lescott vies with Czech forward Stanislav Tecl It's mine: Defender Joleon Lescott vies with Czech forward Stanislav Tecl His chance: As confirmed by Manuel Pellegrini on Sunday, Joe Hart started in goal for Manchester City His chance: As confirmed by Manuel Pellegrini on Sunday, Joe Hart started in goal for Manchester City Get in front: Javi Garcia (right) and Joleon Lescott (left) attempt to block a shot from Milan Petrzela Get in front: Javi Garcia (right) and Joleon Lescott (left) attempt to block a shot from Milan Petrzela Battle: Milner can't get to the ball ahead of Matus Kozacik and Vaclav Prochazka Battle: Milner can't get to the ball ahead of Matus Kozacik and Vaclav Prochazka Previous Article Next Article REAL MADRID YAENDELEZA UBABE ULAYA November 27, 2013, 7:01 pm WINGA Gareth Bale amewaongoza wachezaji 10 wa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Roberto Mancini, Galatasaray, akifunga bao tamu la mpira wa adhabu kipindi cha kwanza. Huku Cristiano Ronaldo akiushuhudia mchezo huo kutoka jukwaa la VIP Uwanja wa Bernabeu, hakuna aliyeweza kumzuia Bale kufunga kwa mpira wa adhabu dakika ya 37. Mabao mengine ya Real yalifungwa na Arbeloa dakika ya 51, Di Maria dakika ya 63 Isco dakika ya 80, wakati bao pekee la Galatasaray lilifungwa na Bulut dakika ya 38. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Arbeloa, Ramos, Pepe, Marcelo/Carvajal dk74, Casemiro/Alonso dk59, Illaramendi, Bale, Isco, Di Maria na Jese/Nacho dk28. Galatasaray: Iscan, Eboue, Gökhan Zan, Chedjou, Nonkeu, Felipe Melo/Gulselam dk88, Inan, Bruma/Sneijder dk63, Umut Bulut, Amrabat/Riera dk67 na Drogba. Unstoppable: Gareth Bale strikes a stunning long-range free-kick to give Real Madrid the lead Over the wall: Galatasaray's Didier Drogba (second from left) jumps to block Bale's free-kick but can't get anywhere near it Over the wall: Galatasaray's Didier Drogba (second from left) jumps to block Bale's free-kick but can't get anywhere near it Back of the net: Goalkeeper Eray Iscan can only watch as Bale's effort flies past him Back of the net: Goalkeeper Eray Iscan can only watch as Bale's effort flies past him Jumping for joy: Bale leaps into the air to celebrate his opening goal Jumping for joy: Bale leaps into the air to celebrate his opening goal Familiar sight: Bale pulls off his trademark heart celebration after putting Madrid 1-0 up Familiar sight: Bale pulls off his trademark heart celebration after putting Madrid 1-0 up Down to 10: Referee William Collum shows Real Madrid defender Sergio Ramos (left) a straight red during the first half Down to 10: Referee William Collum shows Real Madrid defender Sergio Ramos (left) a straight red during the first half Neat finish: Galatasaray's Umut Bulut slides the ball past Iker Casillas to bring his side back on level terms Neat finish: Galatasaray's Umut Bulut slides the ball past Iker Casillas to bring his side back on level terms What a moment: Bulut screams with delight after scoring his side's equaliser at the Bernabeu What a moment: Bulut screams with delight after scoring his side's equaliser at the Bernabeu Unlikely hero: Defender Alvaro Arbeloa (second from left) beats Iscan to put Madrid 2-1 up Unlikely hero: Defender Alvaro Arbeloa (second from left) beats Iscan to put Madrid 2-1 up Previous Article Next Article CHADEMA WAFUNGA MDOMO, DK. SLAA ASEMA CHAMA KINA MAMBO MENGI YA KUFANYA November 27, 2013, 7:05 pm ATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa mjadala kuhusu viongozi wake waliovuliwa nyadhifa zao kwa madai ya kukisaliti chama umefungwa. Viongozi waliovuliwa nyadhifa zao ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, aliyevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo, aliyevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu (CC) na Samson Mwigamba, aliyevuliwa uenyekiti wa Mkoa wa Arusha. Kauli ya kufunga mjadala huo ulioshika kasi kwa takribani wiki moja sasa, ilitangazwa jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. Akizungumza na gazeti hili jana, Dk. Slaa alisema mjadala huo umefungwa, na tayari barua za mashitaka 11 kwenda kwa watuhumiwa zimeshatumwa. “Nataka niwaambie wana CHADEMA wote wanaotumia mitandao na njia nyingine za mawasiliano kwamba mjadala huo sasa umefungwa, hatutaki kusikia, kuona mwanachama yeyote anauendeleza, lakini tutajibu tu pale itakapoonekana kuna upotoshaji,” alisema Dk. Slaa. Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kazi iliyobaki ni kwa watuhumiwa kujibu mashitaka yao ndani ya siku 14 na hatma yao itajulikana kwenye kikao cha Kamati Kuu (CC). Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2010 na kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano, alisema kuna mambo mengi mazito ya kujadili kuliko hilo la mzozo wa Zitto na wenzake. “Tumekumbwa na tatizo la umeme hapa ambao hatujui chanzo, kuna wenzetu wanaendelea kupigwa na kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji, hatuwezi kuendelea na malumbano ambayo hayana tija, CHADEMA ni chama makini na bado kiko imara,” alisema Dk. Slaa. Kauli ya Dk. Slaa itahitimisha mjadala huo ambao tangu watuhumiwa hao walipotangazwa kuvuliwa madaraka, kumekuwa na majibishano kati ya viongozi wa CHADEMA na watuhumiwa hao. Mara baada ya mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza uamuzi wa kuwavua madaraka viongozi hao, Zitto na Dk. Kitila kwa mara ya kwanza walijibu mapigo katika mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo, Zitto na Kitila walitaja sababu walizodai ndizo zimewafanya kuvuliwa nyadhifa zao, ikiwemo suala la ukaguzi wa hesabu za fedha za ruzuku inayotolewa kwa vyama vyenye wabunge, kikiwemo CHADEMA. Zitto alidai kwa muda mrefu amekuwa akizushiwa kupokea rushwa na kukisaliti chama, na kwamba hatoki ndani ya chama hicho kwani nusu ya maisha yake tangu alipojiunga akiwa na miaka 16, hadi sasa ana miaka 37, maisha yake yapo CHADEMA. Kutokana na maelezo hayo ya Zitto na Kitila, CHADEMA juzi walilazimika kuitisha mkutano na kudai kuwa viongozi hao waliovuliwa madaraka, walishindwa kusema ukweli mbele ya waandishi wa habari wiki iliyopita wa kile kilichowafanya wavuliwe nafasi zao. Akizungumza katika mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema Zitto na Dk. Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa masuala ya PAC, uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye operesheni za chama au sababu nyingine, na kwamba walitaja sababu hizo ili kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii. “Walichokifanya kina Zitto na Kitila ni “Diversion” (kubadili mwelekeo) wa mashitaka yao yanayotokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko, ambao ni kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya chama,” alisema Lissu. Aliongeza kuwa CHADEMA ina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na Kamati Kuu, na Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwanini wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika Kamati Kuu. Aidha, Lissu alieleza kuwa Dk. Kitila anapotosha umma kwa kauli yake kuwa Kamati Kuu haina mamlaka ya kumvua nafasi yake ya ujumbe wa Kamati Kuu maana amechaguliwa na Baraza Kuu.CREDIT TANZANIA DAIMA Previous Article Next Article MAMISS WAANZA KUJINOA TAYARI KWA MISS TANZANIA USA PAGEANT JUMAMOSI NOV 30 November 28, 2013, 5:18 am Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant akiwaasa Mamiss Tanzania USA Pageant leo Jumamtano Novemba kwenye hotel ya Marriott Pamela Egbe Messy mratibu wa Miss Africa USA Pageant akiwaelimisha walimbwende MaWinny Casey Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na mratibu wa Miss Tanzania USA Pageant, Asha Nyang'anyi (kulia) Mamiss Tanzania USA Pageant wakimsikiliza Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant alipokuwa Lady Kate, Pamela, Ma Winny na Asha katika picha ya pamoja na Mamiss Tanzania USA. kwa picha zaidi bofya soma zaidi. Sham Manka kutoka Massachusetts akijieleza. Aeesha Kamala kutoka Maryland akijieleza. Joy Kalemera kutoka New Jersey akijieleza. Namala Elias kutoka Maryland akijieleza. Alice Mhina kutoka Maryland akijieleza. Hellena Nyerere kutoka Maryland akijieleza. Faith Kaasha kutoka Alabama akijieleza. Julia Nyerere kutoka Maryland akijieleza. Previous Article Next Article VOTE FOR MOHAMMED DEWJI TO BE THE STYLISH MALE PERSONALITY ON THE SWAHILI FASHION WEEK AWARDS 2013‏ November 28, 2013, 5:18 am MO SFW Banner You can vote online throughhttp://www.swahilifashionweek.com/public/index.php Or by TextingSWFA SMP O3TO15678 Previous Article Next Article Shetta na Diamond Platinum waingia Studio kutengeneza wimbo mpya wa kufungia Mwaka 'Mama Qayllah' November 28, 2013, 5:35 am Ukianza kutaja nyimbo zilizofanya vizuri mwaka 2012 basi lazima utaje wimbo unaofahamika kwa jina la 'Nidanganye Nidanganye' uliyoimbwa na Shetta aliyomshirikisha Naseeb Abdul aka Diamond Platium Sasa habari njema nyingine kutoka kwa Shetta akizungumza na tovuti ya 100.5 leo Novemba 28 amesema kwasasa yupo katika hatua ya maandalizi ya wimbo wake mpya 'Mama Qayllah' aliyomshirikisha Diamond Platinum,wimbo umetengeneza Burn Records chini ya producer 'Sheddy Clever' 'Shetta hapa ama niite Baba Qayllah,kwanza kabla ya yote ningependa kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea vizuri video ya wimbo wangu 'Sina Imani',kwa sasa nipo katika maandalizi ya wimbo wangu mwingine mpya kabisa humo ndani nipo mimi pamoja na Diamond,wimbo unaitwa Mama Qayllah bado upo katika hatua za mwisho za kufanyiwa mixing na Sheddy Clever  wa Burn Records,Kwa hiyo wewe shabiki kaa tayari hapa Baba Qayllah pale Platinum ebu Angalia Mbele'Alisema Shetta. Katika mazungumzo Shetta alidai kuwa huu ndio utakuwa ni wimbo wake wa kufungia Mwaka 2013. CREDIT: TIMES FM Previous Article Next Article HII NDIO CV YA DR. SLAA WA CHADEMA. November 28, 2013, 10:11 am First Name: Dr. Wilbrod Middle Name: Peter Last Name: Slaa Member Type: Constituency Member Constituent: Karatu Political Party: CHADEMA Office Location: P.O. Box 119, Karatu - Arusha Office Phone: +255 784 666995 Ext.: Office Fax: +255 22 2668866 Office E-mail: wslaa@parliament.go.tz Member Status: Current Member Date of Birth 29 October 1948 EDUCATION School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993 1993 CERTIFICATE TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985 1985 CERTIFICATE St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980 1981 ADV DIPLOMA St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977 1981 PHD Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE Itaga Seminary School A-Level Education 1970 1971 HIGH SCHOOL Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966 1969 SECONDARY Karatu Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY Daudi Primary School Primary Education 1961 1961 PRIMARY Kwermusl Primary School(Mbulu) Primary Education 1958 1960 PRIMARY EMPLOYMENT HISTORY Company Name Position From To Tanzania Society for Blind Managing Director 1992 1998 Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985 1991 Diocese of Mbulu Development Director 1982 1985 Diocese of Mbulu Vicar General 1982 1985 Diocese of Mbulu Development Director 1977 1979 Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977 1991 POLITICAL EXPERIENCE Ministry/Political Party/Location Position From To CHADEMA Secretary General 2002 CHADEMA Vice Chairman 1998 2002 CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 Todate CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 - Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch(Rome) 1980 1982 Youth Union -TANU Secretary 1974 1977 TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977 CREDIT: BLOG YA WANANCHI Previous Article Next Article Nani kamkosea Chidi Benz? Tweet zake zaacha utata November 28, 2013, 7:16 pm Hakuna tena kitu kizuri kwa Chidi Benz siku hizi. Kwa muda mrefu rapper huyo ambaye hivi karibuni ametokea kukubalika sana nchini Kenya (thanks kwa mashavu anayopewa na Nonini) ameonekana kutoa yake ya rohoni yanayomuumiza kupitia Twitter. Yeye na Wakazi kuna tatizo? Picha lilianza , baada ya Wakazi kutweet: Na ningependa kusema pia AY, Dimpoz, Ally Kiba, FidQ, Shaa, Cpwaa, Black Rhino, Remi Ongala, Profesa Jay & Lady Jaydee ni other Local heros! Baada ya kuona ujumbe huo wa Wakazi, Chidi alimuuliza kishari ‘nini?’ Wakazi alichuna. Chidi akaamua kuandika: Hujui kuongea huwezi muoga..unaweza kuandika hapa twitter. Nyie ndio mkianza kushindwa mnasifia maadui.#umal** tuu.” Ujumbe huo ulivuta hisia za watu wengi akiwemo Madee aliyeuliza: Rasheeed nani tena kazingua?  Chidi alijibu: Mazafanta wanahisi wanajua kuliko wewe wakati mwenyewe saa zingine unaona hujijui..2 Hata hivyo hatuwezi kuthibitisha kama maneno hayo yalikuwa yakimlenga Wakazi ama mtu mwingine kwakuwa kabla ya hapo tayari alikuwa ameanza kuandika tweets za hasira. “Game ilipo now na propaganda zake inaua vitu vingi tu.sisi tunaonekana tunalalamika ujinga but hatuna maisha mabaya. Viongozi wa nchi sio lazima mdil na bongo freva..haiongezi wewe kufatwa but unatuongezea uadui usio na lazima. Mi natangazwa kwa ubaya tuuuuu.ila nina marafiki bado na wengi wanaongezeka hata hapa.#nakaza roho,” aliandila Chidi. Kunani? Previous Article Next Article Global FC kuwavaa Bagamoyo Veterani kesho November 28, 2013, 11:55 pm Na Shafii Hashim BAADA ya wikiendi iliyopita timu ya Global Publishers FC kuibuka na ushindi wa kibabe wa bao 1-0 dhidi ya Chuo cha Dar es Salaam City (Dacico), kesho Jumamosi timu hiyo inatarajiwa kuelekeza nguvu zake kwenye mechi yao kabambe dhidi ya Bagamoyo Veterani. Mechi hiyo itakayopigwa Bagamoyo, Pwani, ni moja kati ya ziara nyingi za mikoani za kimichezo za timu hiyo zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kukiweka sawa kikosi kwa ajili ya michuano mingi ya kuufunga mwaka 2013 na kuukaribisha 2014. Nahodha wa timu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Mwenge jijini Dar, Phillip Nkini ameliambia gazeti hili kuwa, mara baada ya mechi ya Bagamoyo, ziara yao hiyo itaendelea kwenye mikoa ya Tanga, Morogoro na visiwani Zanzibar. Alisema wakiwa huko, wachezaji wa Global ambao pia ni waandishi wa Gazeti la Championi, watapata fursa ya kuzungumza na wasomaji wao kujua wanahitaji nini zaidi kwenye magazeti ya Championi ili wazidi kulifurahia zaidi gazeti hilo bora la michezo Tanzania. “Baada ya mechi ya Bagamoyo, tutaelekea Tanga, Morogoro na Zanzibar kwa ajili ya kwenda kukipiga huko na kuzungumza na wasomaji wetu,” alisema Nkini. CREDIT: GPL Previous Article Next Article KIBADENI KOCHA MPYA ASHANTI November 29, 2013, 12:02 am KOCHA Mkongwe nchini Abdallah ‘King’ Kibadeni amekubali kutua na kuifundisha Ashanti United ambayo iko katika wakati mgumu. Ashanti iko katika wakati mgumu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa katika nafasi ya 12 kati ya timu 14. Habari za uhakika kutoka ndani ya Ashanti zimeeleza, tayari mazungumzo kati ya Kibadeni na kocha huyo yamefanyika, naye ameridhia kutua huko. “Tayari mazungumzo yamefanyika, naweza kusema ni asilimia 90 tuko katika makubaliano na Kibadeni na amekubali kuja kuifundisha timu yetu. Amesema lile agizo la Rage kumrudisha yeye amelikataa na hatabaki Simba,” kilieleza chanzo. “Kwa kuwa ametuhakikishia, basi tumeanza kuandaa kila anachotaka na tunasubiri tu amalizane na Simba kuchukua haki yake ili aanze kazi hapa Ashanti.” Alipotafutwa Kibadeni, jana mchana, alikiri kufanya mazungumzo na Ashanti lakini akasisitiza suala hilo litabaki kuwa siri. “Kweli siwezi kubaki Simba, huo ni ukweli. Lakini kuhusiana na Ashanti na mambo mengine yote ya Simba nitayazungumza Jumamosi. “Nimeitisha mkutano na waandishi wa habari, nimewaomba waje kwangu Madale, saa nne kamili asubuhi. Nitaeleza kila kitu kuhusiana na Simba na hata Ashanti, hivyo leo siwezi kuzungumza zaidi,” alisema Kibadeni. Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ walifukuzwa kazi na kamati ya utendaji lakini mwenyekiti aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage akawarudisha na kujirudisha madarakani akisema kamati hiyo haikufuata katiba. CREDIT: GPL Previous Article Next Article NBA INALIPA SI MCHEZO November 29, 2013, 12:05 am Previous Article Next Article ALICHOKISEMA YULE PRODUCER ALIYEFUKUZWA KAZI NA WEMA SEPETU KWA UZINZI November 29, 2013, 5:46 pm Baada ya juzi kati kuripotiwa habari ya aliyekuwa producer ama mtengenezaji wa vipindi vya Wema Sepetu Chidi Mohamed kufukuzwa kazi kutokana na kulitumia gari la kampuni kama sehemu yake ya kuvunjia amri ya sita na wadada wa mjini, hatimaye katika pitapita zetu za mtandaoni tuliweza kukutana na kauli ya producer huyo akizungumzia habari hiyo ya yeye kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Endless Fame ya wema sepetu. Chidi mwenyewe anasema kuwa habari hizo si za kwel na ni kwamba wote walioandika wamepanga kumchafua tuu kwa kuogopa kuwa anaweza kuyaniika mambo mazito yanayoendelea huko endless Fame Kwa mujibu wa chidi anasema kuwa yeye ameondoka kwenye Kampuni hiyo siyo kwa sababu ya uzinzi ngani ya gari kama ilivyoripotiwa bali ni kutokana na sababu hizi kuu mbili. 1. Ameona hamna jipya na wala hamna maendeleo yoyote ndani ya Kampuni hiyo ndio maana ameamua kuondoka 2.Wafanyakazi wa Endless Fame hawalipwi kabisa ndio maana yeye akaamua kujitoa kwani anafanya kazi bure na pia sio yeye peke yake aliyeondoka bali kuna wafanyakazi zaidi ya watatu walioondoka kwenye kampuni hiyo ila nashangaa ni kwanini wameamua kumchafua yeye? Bado tunafanya mawasiliano na Endless Fame ili tujue kama daia haya ni ya kweli au la CREDIT: BONGO MOVIE Previous Article Next Article RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOKEA KOMBE LA DUNIA JIJINI MWANZA, LEO NI DAR. November 29, 2013, 6:21 pm Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akilifunua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo wa Kirumba jijini Mwanza jana jioni baada ya kulipokea Kombe hilo lililotua nchini kwa mara ya pili, ambapo leo wananchi watapata fursa ya kupia nalo picha. Rais Kikwete, akilinyanyua Kombe hilo kwa furaha baada ya kuzindua rasmi shambra shambra za ujio wake nchini katika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza jana jioni. rai Kikwete, akifurahia hukua kiwa ameliinua Kombe hilo juu kuwaonyesha wananchi waliojitokeza kwenye Uwanja wa Kirumba kulipokea. Wananchi wa Jiji la dar es Salaam, leo watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo katika Uwanja wa Taifa. Previous Article Next Article WEMA AMUANZISHIA TIMBWILI FUNDI WAKE November 29, 2013, 6:24 pm BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu ametengeneza habari mpya kama kawaida yake. Safari hii amemuanzishia timbwili zito fundi wake aliyefahamika kwa jina moja la James. Wema Isaac Sepetu. Akizungumza kupitia kipindi chake cha In My Shoes mapema wiki hii, Wema ambaye hachukii ukimuita Madam, aliweka bayana kuwa tukio hilo ambalo lilitokea siku za nyuma lilimkera kwa sababu fundi huyo alimuamini kuwa atamfanyia ukarabati mzuri wa nyumba yake, badala yake akamharibia. Siku ya tukio, Wema aliyekuwa amehama kwa muda kupisha ukarabati wa nyumba hiyo, baada ya fundi kujiridhisha kuwa amekamilisha ujenzi, alimuita Wema akakague ndipo mtiti ulipoanza. Alimtukana fundi huyo, akamfokea vya kutosha akidai hajaridhishwa na ukarabati alioufanya. “This is my house, kwa nini umefanya vibaya? Sijapenda, sasa hivi ndiyo nini? Rangi gani hii umepaka? Yaani umeniharibia kila kitu, sipendi kuharibiwa kabisa nyumba yangu…” alifoka Wema. Licha ya Meneja wa Wema, Martin Kadinda kuwepo nyumbani hapo na kumsihi wampe siku mbili fundi huyo ili arudie ukarabati, Madam aliendelea kuvurumisha ‘mitusi’ kama aliyechanganyikiwa. Sini hiyo ya varangati ilioneshwa ‘live’ kupitia kipindi chake hicho kinachorushwa na Runinga ya East Africa ambapo fundi huyo alionekana akimwaga machozi kisha kuondoka nyumbani hapo kwa unyonge baada ya kukosa muafaka.

Blog